Maadhimisho Ya Maulidi Ni Kujifananisha Na Manaswara

Kuhusu nukuu ya ar-Rifaa'iy ya as-Sakhaawiy ambaye amesema: "Ikiwa wakristo wamefanya Krismasi kuwa sikukuu, Waislamu wana haki zaidi juu yake kwa Mtume wao." hakuna shaka kwamba maadhimisho ya Maulidi yamejengeka juu ya kujifananisha na manaswara ambao wamechukua kuzaliwa kwa Masiyh kuwa ni sikukuu. Hili linathibitisha maneno ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam): "Mtafuata desturi (mwenendo) za waliokuwa kabla yenu shibri kwa shibri na pima kwa pima hata wakiingia katika shimo la mburukenge (yaani ndani ya shimo lenye mnyama anayeweza kukudhuru) mutaingia nao.” Tukasema: “Je, unakusudia mayahudi na manasara?” Akasema: “Ni nani wengine ikiwa si wao?" (Imepokelewa na Imaam Ahmad, al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwa Abu Sa'iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu 'anhu) Wakati mtu anajua kuwa maadhimisho ya Maulidi ya wajinga msingi wake umejengeka juu ya kujifananisha na manaswara, basi mtu anapaswa pia kujua kwamba imekatazwa vikali kujifananisha na manaswara na washirikina. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: “Yule anayejifananisha na watu basi [mtu huyo] ni katika wao.” Imepokelewa na Imaam Ahmad na Abu Daawuud kutoka kwa 'Abdullaah bin 'Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Mwandishi: 'Allaamah Hamuud bin 'Abdillaah at-Tuwayjiriy ar-Radd al-Qawiy, uk. 25-26

Kuhusu nukuu ya ar-Rifaa’iy ya as-Sakhaawiy ambaye amesema:

“Ikiwa wakristo wamefanya Krismasi kuwa sikukuu, Waislamu wana haki zaidi juu yake kwa Mtume wao.”

hakuna shaka kwamba maadhimisho ya Maulidi yamejengeka juu ya kujifananisha na manaswara ambao wamechukua kuzaliwa kwa Masiyh kuwa ni sikukuu. Hili linathibitisha maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):

“Mtafuata desturi (mwenendo) za waliokuwa kabla yenu shibri kwa shibri na pima kwa pima hata wakiingia katika shimo la mburukenge (yaani ndani ya shimo lenye mnyama anayeweza kukudhuru) mutaingia nao.” Tukasema: “Je, unakusudia mayahudi na manasara?” Akasema: “Ni nani wengine ikiwa si wao?” (Imepokelewa na Imaam Ahmad, al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwa Abu Sa’iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Wakati mtu anajua kuwa maadhimisho ya Maulidi ya wajinga msingi wake umejengeka juu ya kujifananisha na manaswara, basi mtu anapaswa pia kujua kwamba imekatazwa vikali kujifananisha na manaswara na washirikina. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kasema:

“Yule anayejifananisha na watu basi [mtu huyo] ni katika wao.”

Imepokelewa na Imaam Ahmad na Abu Daawuud kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa).

Mwandishi: ‘Allaamah Hamuud bin ‘Abdillaah at-Tuwayjiriy
ar-Radd al-Qawiy, uk. 25-26


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 24th, October 2013