Kuwaomba Mawalii Waliokufa

Swali La Kwanza: Waabudu makaburi wanasema ya kwamba mawalii wako hai kwenye makaburi yao na kwamba wako hai kama mashahidi. Twaomba majibu ya haya? ´Allaamah al-Fawzaan: Mashahidi wao wako hai kwenye makaburi yao, ama mawalii hatujui kwamba wako hai. Hata lau ingelithibiti ya kwamba wako hai, haya ni maisha ya Barzakhiyyah na sio kama maisha yao ya duniani. Hawaombwi kitu. Na kwa ajili hiyo, vinagawanywawalivyoviacha, wanaolewa wake zao, wanazikwa chini ya udongo. Haya ni [maisha] maalum ya Barzakhiyyah na hayana mafungamano yoyote na ya dunia. Swali La Pili: Wanatwambia "mawalii hawamiliki chochote katika nafsi zao, lakini Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) yeye ndiye Kawapa nguvu na uwezo kamili. ´Allaamah al-Fawzaan: Ewe ndugu! Maadamu Allaah ndiye Kawapa na wewe umekubali hilo, muombe Allaah na wala usiwaombe. Hili ni mfano wa mtu mmoja aliyemwambia mwanachuoni, nyinyi mnawachukia mawalii. Na Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema: وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتًا ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ "Na wala usiwadhanie kabisa wale ambao wameuawa katika njia ya Allaah ni wafu, bali wahai, kwa Mola wao wanaruzukiwa." (03:169) Akamwambia - haikuwa hata mwanachuoni bali alikuwa ni mtu ´Aamiy (ambaye si msomi) - "Je, Allaah Kasema: "... bali wahai, kwa Mola wao wanaruzuku" au Kasema "... wanaruzukiwa"? Akasema "Hapana, wanaruzukiwa". Akamwambia "Basi kama ni hivyo mimi namuomba yule ambaye Kawaruzuku Aniruzuku." Akakasirika (yule mshirikina), na huyu ni mtu ambaye si msomi. Na kwa hili kasema Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab katika kitabu chake Kashf-us-Shubuhaat: "Na mtu ´Aamiy (ambaye si msomi) katika Muwahhidiyn anashinda [watu] elfu katika wanachuoni wa watu hawa." Kwa kuwa mtu huyu ana Fitrah iliyo ya salama hata kama ni ´Aamiy, na huyu Fitrah yake imechafuka. A´udhubi Allaah.

Swali La Kwanza:
Waabudu makaburi wanasema ya kwamba mawalii wako hai kwenye makaburi yao na kwamba wako hai kama mashahidi. Twaomba majibu ya haya?

´Allaamah al-Fawzaan:
Mashahidi wao wako hai kwenye makaburi yao, ama mawalii hatujui kwamba wako hai. Hata lau ingelithibiti ya kwamba wako hai, haya ni maisha ya Barzakhiyyah na sio kama maisha yao ya duniani. Hawaombwi kitu. Na kwa ajili hiyo, vinagawanywawalivyoviacha, wanaolewa wake zao, wanazikwa chini ya udongo. Haya ni [maisha] maalum ya Barzakhiyyah na hayana mafungamano yoyote na ya dunia.

Swali La Pili:
Wanatwambia “mawalii hawamiliki chochote katika nafsi zao, lakini Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) yeye ndiye Kawapa nguvu na uwezo kamili.

´Allaamah al-Fawzaan:
Ewe ndugu! Maadamu Allaah ndiye Kawapa na wewe umekubali hilo, muombe Allaah na wala usiwaombe. Hili ni mfano wa mtu mmoja aliyemwambia mwanachuoni, nyinyi mnawachukia mawalii. Na Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema:

وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتًا ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ
“Na wala usiwadhanie kabisa wale ambao wameuawa katika njia ya Allaah ni wafu, bali wahai, kwa Mola wao wanaruzukiwa.” (03:169)

Akamwambia – haikuwa hata mwanachuoni bali alikuwa ni mtu ´Aamiy (ambaye si msomi) – “Je, Allaah Kasema: “… bali wahai, kwa Mola wao wanaruzuku” au Kasema “… wanaruzukiwa”? Akasema “Hapana, wanaruzukiwa”. Akamwambia “Basi kama ni hivyo mimi namuomba yule ambaye Kawaruzuku Aniruzuku.” Akakasirika (yule mshirikina), na huyu ni mtu ambaye si msomi.

Na kwa hili kasema Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab katika kitabu chake Kashf-us-Shubuhaat:

“Na mtu ´Aamiy (ambaye si msomi) katika Muwahhidiyn anashinda [watu] elfu katika wanachuoni wa watu hawa.”

Kwa kuwa mtu huyu ana Fitrah iliyo ya salama hata kama ni ´Aamiy, na huyu Fitrah yake imechafuka. A´udhubi Allaah.