Kuna Mitume Na Majini Wanaotokamana Na Majini?

Je, kuna Mtume au Nabii anayetokamana na majini? Kuna waliosema, imepokelewa kutoka kwa adh-Dhwahhaak bin Muzaahim, Mujaahid na wengine akiwemo Ibn ´Abbaas ya kwamba utume unakuwa kwa mwaadamu peke yao. Ama majini kunakuwa waonyaji tu kama ilivyo katika Aayah: فَلَمَّا قُضِيَ وَلَّوْا إِلَىٰ قَوْمِهِم مُّنذِرِينَ قَالُوا يَا قَوْمَنَا إِنَّا سَمِعْنَا كِتَابًا أُنزِلَ مِن بَعْدِ مُوسَىٰ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ وَإِلَىٰ طَرِيقٍ مُّسْتَقِيمٍ يَا قَوْمَنَا أَجِيبُوا دَاعِيَ اللَّـهِ “Nyamazeni [msikilize]” Ilipokwisha somwa; waligeuka kurudi kwa watu wao wakiwaonya wakasema: “Enyi watu wetu! Hakika sisi tumesikia Kitabu kilichoteremsha baada ya Muwsaa, kinachosadikisha yaliyo kabla yake, kinaongoza kwenye haki na kuelekea njia iliyonyooka. “Enyi watu wetu! Mwitikieni mlinganiaji wa Allaah."" (46:29-31) Unabii na Utume unakuwa kwa wanaadamu. Majini wanakuwa na waonyaji tu. Kuhusiana na Kauli Yake (Ta´ala): يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ "[Siku ya Qiyaamah wataambiwa]: “Enyi wenzi wa majini na wanadamu! Je hawajakufikieni Mtume miongoni mwenu."" (06:130) sio lazima iwe Mtume ni mwenye kutokamana na wao wote wawili, bali ni kutokamana na mmoja katika wao ambao ni wanaadamu. Wengine wakasema hakuna kizuizi juu ya hilo. Allaah (Ta´ala) amesema: يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ "[Siku ya Qiyaamah wataambiwa]: “Enyi wenzi wa majini na wanadamu! Je hawajakufikieni Rasuli miongoni mwenu." Dhahiri yake ni kwamba katika majini kuna Mitume pia. Mzungumzaji: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy Chanzo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/149) Toleo la: 10.11.2015 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Je, kuna Mtume au Nabii anayetokamana na majini? Kuna waliosema, imepokelewa kutoka kwa adh-Dhwahhaak bin Muzaahim, Mujaahid na wengine akiwemo Ibn ´Abbaas ya kwamba utume unakuwa kwa mwaadamu peke yao. Ama majini kunakuwa waonyaji tu kama ilivyo katika Aayah:

فَلَمَّا قُضِيَ وَلَّوْا إِلَىٰ قَوْمِهِم مُّنذِرِينَ قَالُوا يَا قَوْمَنَا إِنَّا سَمِعْنَا كِتَابًا أُنزِلَ مِن بَعْدِ مُوسَىٰ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ وَإِلَىٰ طَرِيقٍ مُّسْتَقِيمٍ يَا قَوْمَنَا أَجِيبُوا دَاعِيَ اللَّـهِ
“Nyamazeni [msikilize]” Ilipokwisha somwa; waligeuka kurudi kwa watu wao wakiwaonya wakasema: “Enyi watu wetu! Hakika sisi tumesikia Kitabu kilichoteremsha baada ya Muwsaa, kinachosadikisha yaliyo kabla yake, kinaongoza kwenye haki na kuelekea njia iliyonyooka. “Enyi watu wetu! Mwitikieni mlinganiaji wa Allaah.”” (46:29-31)

Unabii na Utume unakuwa kwa wanaadamu. Majini wanakuwa na waonyaji tu. Kuhusiana na Kauli Yake (Ta´ala):

يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ
“[Siku ya Qiyaamah wataambiwa]: “Enyi wenzi wa majini na wanadamu! Je hawajakufikieni Mtume miongoni mwenu.”” (06:130)

sio lazima iwe Mtume ni mwenye kutokamana na wao wote wawili, bali ni kutokamana na mmoja katika wao ambao ni wanaadamu.

Wengine wakasema hakuna kizuizi juu ya hilo. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ
“[Siku ya Qiyaamah wataambiwa]: “Enyi wenzi wa majini na wanadamu! Je hawajakufikieni Rasuli miongoni mwenu.”

Dhahiri yake ni kwamba katika majini kuna Mitume pia.

Mzungumzaji: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
Chanzo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/149)
Toleo la: 10.11.2015
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Mashetani na Majini
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Tuesday 10th, November 2015