Kujifunza Mwenyewe – Maradhi Khatari Ya leo

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab kasema: "34- Usiamini Dini yako katika vitabu na wale wanaojinasibisha kwa elimu." Imaam al-Fawzaan: Usiamini vitabu moja kwa moja. Ssiviamini. Kwa kuwa kuna haki na batili. Usiviamini vitabu. Bali rejea kwa maulamaa (wanachuon) waliobobea katika elimu. Usichukue elimu yako tu katika vitabu, au ukasoma kwenye vitabu vyenyewe. Baadhi ya watu wanahifadhi mujaladi na maandishi, lakini hawafahamu yaliyomo ndani yake na wala hawajui maana yake. Kwa kuwa hawakusoma kwa maulamaa ambao wanasherehesha na wanabainisha muradi wake. Wanaweza kufahamu ufahamu ambao ni wakimakosa. Hili ni khatari! Usiamini hivi vitabu. Vitabu ni njia tu katika elimu. Usiviamini katika kujifunza kwako. Si vitabu vyote vinakuwa sahihi. Hata kama kitabu ni sahihi ufahamu wako una mpaka. Fahamu inatofautiana hata kama kitabu kitakuwa sahihi. Je Khawaarij hawakupotea nao ni walikuwa ni wenye kuhifadhi Qur-aan na wanasimama na kuisoma usiku katika Tahajjud wakiswali? Lakini wamepotea. Allaah Atulinde. Kwa kuwa hawafahamu maana ya Qur-aan na hawakuchukua elimu kwa maulamaa. Walijitenga na Maswahabah na wakatosheka na kusoma Qur-aan na ufahamu wao kivyao. Ndo maana wamepatwa na yaliyowapata. Na haya maradhi ya leo ni khatari. Mtu kudhani kuwa anajua ni maradhi khatari, nako ni kuchukua elimu kwenye vitabu au kwa watu wasiofahamu kwa wale wanaodhani kuwa wanajua na wanaoanza. Hii ni khatari kwa mtu mwenyewe na ni khatari kwa Ummah. Kwa kuwa atataka aanze kutoa Fatwa, aanze kufasiri Qur-aan au kufasiri Sunnah apoteze watu.

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab kasema:

“34- Usiamini Dini yako katika vitabu na wale wanaojinasibisha kwa elimu.”

Imaam al-Fawzaan:

Usiamini vitabu moja kwa moja. Ssiviamini. Kwa kuwa kuna haki na batili. Usiviamini vitabu. Bali rejea kwa maulamaa (wanachuon) waliobobea katika elimu. Usichukue elimu yako tu katika vitabu, au ukasoma kwenye vitabu vyenyewe. Baadhi ya watu wanahifadhi mujaladi na maandishi, lakini hawafahamu yaliyomo ndani yake na wala hawajui maana yake. Kwa kuwa hawakusoma kwa maulamaa ambao wanasherehesha na wanabainisha muradi wake. Wanaweza kufahamu ufahamu ambao ni wakimakosa. Hili ni khatari! Usiamini hivi vitabu. Vitabu ni njia tu katika elimu. Usiviamini katika kujifunza kwako. Si vitabu vyote vinakuwa sahihi. Hata kama kitabu ni sahihi ufahamu wako una mpaka. Fahamu inatofautiana hata kama kitabu kitakuwa sahihi. Je Khawaarij hawakupotea nao ni walikuwa ni wenye kuhifadhi Qur-aan na wanasimama na kuisoma usiku katika Tahajjud wakiswali? Lakini wamepotea. Allaah Atulinde. Kwa kuwa hawafahamu maana ya Qur-aan na hawakuchukua elimu kwa maulamaa. Walijitenga na Maswahabah na wakatosheka na kusoma Qur-aan na ufahamu wao kivyao. Ndo maana wamepatwa na yaliyowapata. Na haya maradhi ya leo ni khatari. Mtu kudhani kuwa anajua ni maradhi khatari, nako ni kuchukua elimu kwenye vitabu au kwa watu wasiofahamu kwa wale wanaodhani kuwa wanajua na wanaoanza. Hii ni khatari kwa mtu mwenyewe na ni khatari kwa Ummah. Kwa kuwa atataka aanze kutoa Fatwa, aanze kufasiri Qur-aan au kufasiri Sunnah apoteze watu.