Kuishi Katika Miji Ya Makafiri

Kwa kuwa ni miji ya Makafiri, na Makafiri wanawashajihisha ndugu zao Makafiri - nao ni kama wao. وَدُّواْ لَوْ تَكْفُرُونَ كَمَا كَفَرُو “Wanapenda lau kuwa nanyi mnge kufuru kama walivyokufuru wao.” (04:89) Kwahiyo hawa watu wanataka kutupoteza - tunamuomba Allaah afya na usalama. Kama Alivyosema Allaah (Jalla wa 'Alaa): وَاللّهُ يُرِيدُ أَن يَتُوبَ عَلَيْكُمْ وَيُرِيدُ الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الشَّهَوَاتِ أَن تَمِيلُواْ مَيْلاً عَظِيمًا يُرِيدُ اللّهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمْ وَخُلِقَ الإِنسَانُ ضَعِيفًا “Na Allaah anataka kukurejezeni kwenye utiifu Wake, na wanaotaka kufuata matamanio wanataka mkengeuke makengeuko makubwa. Allaah Anataka kukupunguzieni taabu, na mwanaadamu ameumbwa dhaifu.” (04:27-28) Hawa watu hawataki jengine ila hili. وَلَن تَرْضَى عَنكَ الْيَهُودُ وَلاَ النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ “Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate dini zao.” (02:120) وَدُّواْ لَوْ تَكْفُرُونَ كَمَا كَفَرُواْ فَتَكُونُونَ سَوَاء فَلاَ تَتَّخِذُواْ مِنْهُمْ أَوْلِيَاء “Wanapenda lau kuwa nanyi mnge kufuru kama walivyokufuru wao, ili muwe sawa sawa. Basi msiwafanye marafiki miongoni.” (04:89) واْ إِنَّ الْكَافِرِينَ كَانُواْ لَكُمْ عَدُوًّا مُّبِينًا “Hakika makafiri ni maadui zenu walio wazi wazi.” (04:101) Kwa hiyo hawa watu hili ndilo wanalotaka na wamekwishafanikiwa katika suala la mke na mume na tunamuomba Allaah afya na usalama. Hili ndilo linaloendelea enyi ndugu - kuishi kwenye miji ya kikafiri ni jambo hatari sana. Na linatisha kwa watu wake [Waislamu] wanaoishi huko upotofu kuwafika. Na Mtume (Swala Allaahu 'alayhi wa sallam) anasema: "Mimi niko mbali na kila Muislamu ambaye anaishi miongoni mwa Washirikina." (Tukauliza kwa nini ewe Mtume wa Allaah?" akajibu: "Moto wao hutoonekana baina yao." Yaani kwa mfano unaishi kwenye jangwa, ungelikuwa mbali ya kila mmoja kiasi ambacho akiwasha moto usingeliweza kumuona wewe, na wewe ungeliwasha moto naye [kafiri] pia asingelikuona." Kunakuwa baina yako wewe na yeye masafa ambayo huwezi kuona uso wake, [madhara] unageuka kuwa laini kwake, unakuwa na huruma naye, hufai kuwa na urafiki naye, kumvumilia, (na ukifanya hivi) mambo yote yanakuwa kawaida. Na namna hivyo inakuwa wakati Muislamu akisafiri kwenda kwenye mji wa kikafiri. Siku zinavyoanza ataanza kuchukia maovu, atapobakia siku kadhaa atachukia maovu zaidi, anapobakia miezi kadhaa mingine chuki yake itapungua na kuwa mdhaifu na mwisho wake chuki itatoweka kabisa na huenda baada ya hayo akaanza kufanya ambavyo Makafiri wanavyofanya kama wao. Nanasihi ndugu zetu ambao wanaishi kwenye miji ya makafiri wamuogope Allaah (Jalla wa 'Alaa) wenyewe, na kwa watoto wao - wanaume na wanawake, kwa kuwa watoto - sawa wanaume na wanawake wanapofikisha miaka kumi na nane, mzazi wake hana mamlaka juu yake. Binti anapiga kona, anatoka na atafanya apendacho. Akizini hakuna kitu juu yake - huna mamlaka juu yake. Ukimtamkia nawe ni baba yake, atakupeleka mahakamani [serikalini] na watakutupa jela - basi huna neno! Hali kadhalika mtoto wako, ataua n,k ukijaribu kunyoosha mkono wako [na kumnasihi] watakutupa jela. Ipi faida ya kuishi kwenye miji hiyo? Ni wajibu kwa Waislamu wafanye Hijrah kuhamia kwenye miji ya Waislamu kadiri na wawezavyo. Waislamu wengi wanatafuta [kuishi] mamlaka [Saudia] tunasema hili ni jambo zuri ikiwa litawezekana, lakini ikiwa haliwezekani mji wowote wa Waislamu ni bora kwako kuishi kuliko kubakia kwenye mji wa makafiri. Na kwa masikitiko makubwa kuna jambo lingine linaloeleweka vibaya katika suala hili. Wanaita wale wanaokwenda kwenye miji ya makafiri kuwa ni "Muhaajiruun" kama tulivyosikia kwenye habari meli ilienda kaskazini mwa Afrika, wakaua Muhaajiruun njiani wakielekea Italia" wakatangaza na kusema "Muhaajiruun 90 au 40 wamepatikana wamekufa" je, hawa ni Muhaajiruun? Hijrah ni kutoka kwenye mji wa Shirki na kwenda (kuhamia) kwenye mji wa Waislamu, na si [mtu] kutoka kwenye mji wa Waislamu na kwenda kwenye mji wa Shirki - hili ni kosa. Hijrah ni [mtu] kutoka kwenye mji wa Shirki na kwenda kwenye Mji wa Waislamu. Hawa watu sio Muhaajiruun - hawa watu wameihama dini yao na kwenda kwenye miji ya kufuru. Na jambo lingine ni kuwa hawa watu hawaendi kwa misingi ya Kishari'ah sahihi; kama kwenda kujifunza elimu ambayo haipatikani kwenye miji ya Waislamu au kwenda kujitibisha kwa maradhi ambayo haikupatikana dawa kwenye miji ya Waislamu au biashara ya dharurah imewajibika kwao kusafiri, hapana [wao sivyo]! Wanaenda kwa mambo ambayo watajipumbaza kwayo kama Ulaya au Amerika, na watu waovu Dajjal ambao wanawahamasisha kwa hili kwenye vyombo vya habari na matovuti, unabonyeza kwenye link inakwambia "Mabruuk! Umepata kibali cha kuweza kuishi US - wasiliana nasi." Wanaweza hata kukuibia. Ni wajibu kwa ndugu zetu wamuogope Allaah (Jalla wa 'Alaa) na wasiishi kwenye miji ya Makafiri ila kwa dharurah, na dharurah inachukuliwa kadiri ya umuhimu wake, na pindi dharurah inapoondoka haijuzu kwao kubaki [kwenye hio miji ya Makafiri].

Kwa kuwa ni miji ya Makafiri, na Makafiri wanawashajihisha ndugu zao Makafiri – nao ni kama wao.

وَدُّواْ لَوْ تَكْفُرُونَ كَمَا كَفَرُو
“Wanapenda lau kuwa nanyi mnge kufuru kama walivyokufuru wao.” (04:89)

Kwahiyo hawa watu wanataka kutupoteza – tunamuomba Allaah afya na usalama. Kama Alivyosema Allaah (Jalla wa ‘Alaa):

وَاللّهُ يُرِيدُ أَن يَتُوبَ عَلَيْكُمْ وَيُرِيدُ الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الشَّهَوَاتِ أَن تَمِيلُواْ مَيْلاً عَظِيمًا يُرِيدُ اللّهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمْ وَخُلِقَ الإِنسَانُ ضَعِيفًا
“Na Allaah anataka kukurejezeni kwenye utiifu Wake, na wanaotaka kufuata matamanio wanataka mkengeuke makengeuko makubwa. Allaah Anataka kukupunguzieni taabu, na mwanaadamu ameumbwa dhaifu.” (04:27-28)

Hawa watu hawataki jengine ila hili.

وَلَن تَرْضَى عَنكَ الْيَهُودُ وَلاَ النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ
“Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate dini zao.” (02:120)

وَدُّواْ لَوْ تَكْفُرُونَ كَمَا كَفَرُواْ فَتَكُونُونَ سَوَاء فَلاَ تَتَّخِذُواْ مِنْهُمْ أَوْلِيَاء
“Wanapenda lau kuwa nanyi mnge kufuru kama walivyokufuru wao, ili muwe sawa sawa. Basi msiwafanye marafiki miongoni.” (04:89)

واْ إِنَّ الْكَافِرِينَ كَانُواْ لَكُمْ عَدُوًّا مُّبِينًا
“Hakika makafiri ni maadui zenu walio wazi wazi.” (04:101)

Kwa hiyo hawa watu hili ndilo wanalotaka na wamekwishafanikiwa katika suala la mke na mume na tunamuomba Allaah afya na usalama.

Hili ndilo linaloendelea enyi ndugu – kuishi kwenye miji ya kikafiri ni jambo hatari sana. Na linatisha kwa watu wake [Waislamu] wanaoishi huko upotofu kuwafika. Na Mtume (Swala Allaahu ‘alayhi wa sallam) anasema:

“Mimi niko mbali na kila Muislamu ambaye anaishi miongoni mwa Washirikina.” (Tukauliza kwa nini ewe Mtume wa Allaah?” akajibu: “Moto wao hutoonekana baina yao.”

Yaani kwa mfano unaishi kwenye jangwa, ungelikuwa mbali ya kila mmoja kiasi ambacho akiwasha moto usingeliweza kumuona wewe, na wewe ungeliwasha moto naye [kafiri] pia asingelikuona.”
Kunakuwa baina yako wewe na yeye masafa ambayo huwezi kuona uso wake, [madhara] unageuka kuwa laini kwake, unakuwa na huruma naye, hufai kuwa na urafiki naye, kumvumilia, (na ukifanya hivi) mambo yote yanakuwa kawaida.

Na namna hivyo inakuwa wakati Muislamu akisafiri kwenda kwenye mji wa kikafiri. Siku zinavyoanza ataanza kuchukia maovu, atapobakia siku kadhaa atachukia maovu zaidi, anapobakia miezi kadhaa mingine chuki yake itapungua na kuwa mdhaifu na mwisho wake chuki itatoweka kabisa na huenda baada ya hayo akaanza kufanya ambavyo Makafiri wanavyofanya kama wao.

Nanasihi ndugu zetu ambao wanaishi kwenye miji ya makafiri wamuogope Allaah (Jalla wa ‘Alaa) wenyewe, na kwa watoto wao – wanaume na wanawake, kwa kuwa watoto – sawa wanaume na wanawake wanapofikisha miaka kumi na nane, mzazi wake hana mamlaka juu yake. Binti anapiga kona, anatoka na atafanya apendacho.

Akizini hakuna kitu juu yake – huna mamlaka juu yake. Ukimtamkia nawe ni baba yake, atakupeleka mahakamani [serikalini] na watakutupa jela – basi huna neno! Hali kadhalika mtoto wako, ataua n,k ukijaribu kunyoosha mkono wako [na kumnasihi] watakutupa jela. Ipi faida ya kuishi kwenye miji hiyo?

Ni wajibu kwa Waislamu wafanye Hijrah kuhamia kwenye miji ya Waislamu kadiri na wawezavyo. Waislamu wengi wanatafuta [kuishi] mamlaka [Saudia] tunasema hili ni jambo zuri ikiwa litawezekana, lakini ikiwa haliwezekani mji wowote wa Waislamu ni bora kwako kuishi kuliko kubakia kwenye mji wa makafiri.

Na kwa masikitiko makubwa kuna jambo lingine linaloeleweka vibaya katika suala hili. Wanaita wale wanaokwenda kwenye miji ya makafiri kuwa ni “Muhaajiruun” kama tulivyosikia kwenye habari meli ilienda kaskazini mwa Afrika, wakaua Muhaajiruun njiani wakielekea Italia” wakatangaza na kusema “Muhaajiruun 90 au 40 wamepatikana wamekufa” je, hawa ni Muhaajiruun?

Hijrah ni kutoka kwenye mji wa Shirki na kwenda (kuhamia) kwenye mji wa Waislamu, na si [mtu] kutoka kwenye mji wa Waislamu na kwenda kwenye mji wa Shirki – hili ni kosa. Hijrah ni [mtu] kutoka kwenye mji wa Shirki na kwenda kwenye Mji wa Waislamu. Hawa watu sio Muhaajiruun – hawa watu wameihama dini yao na kwenda kwenye miji ya kufuru.

Na jambo lingine ni kuwa hawa watu hawaendi kwa misingi ya Kishari’ah sahihi; kama kwenda kujifunza elimu ambayo haipatikani kwenye miji ya Waislamu au kwenda kujitibisha kwa maradhi ambayo haikupatikana dawa kwenye miji ya Waislamu au biashara ya dharurah imewajibika kwao kusafiri, hapana [wao sivyo]!

Wanaenda kwa mambo ambayo watajipumbaza kwayo kama Ulaya au Amerika, na watu waovu Dajjal ambao wanawahamasisha kwa hili kwenye vyombo vya habari na matovuti, unabonyeza kwenye link inakwambia “Mabruuk! Umepata kibali cha kuweza kuishi US – wasiliana nasi.” Wanaweza hata kukuibia.

Ni wajibu kwa ndugu zetu wamuogope Allaah (Jalla wa ‘Alaa) na wasiishi kwenye miji ya Makafiri ila kwa dharurah, na dharurah inachukuliwa kadiri ya umuhimu wake, na pindi dharurah inapoondoka haijuzu kwao kubaki [kwenye hio miji ya Makafiri].


  • Author: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Kitengo: Uncategorized , Tawhiyd na ´Aqiydah
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 18th, October 2013