Kuhusu sisi


Wanachuoni.com ni tovuti iliyofunguliwa na kuendeshwa na wanafunzi kutoka Afrika mashariki. Lengo lake kuu ni kutumika kama mabalozi wa wanachuoni (Allaah awarehemu wale waliotangulia mbele za haki na awahifadhi walioko hii leo). Ni tovuti iliyojengeka juu ya Qur-aan na Sunnah kwa ufahamu wa Maswahabah, maimamu wa karne tatu bora za mwanzo na wale wenye kuwafuata kwa wema. Hili ni kutokana na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Jilazimieni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu baada yangu.”

Vilevile itambulike kuwa tovuti hii imesalimika kabisa kutokamana na ukundi, fikra za kigeni, upetukaji, mambo ya uzushi, ufuataji kipofu na kasumba za kimadhehebu na kitaifa. Hili ni kutokana na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Tahadharini na mambo yaliyozuliwa. Hakika kila kilichozuliwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.”

”Ummah wangu utagawanyika mapote sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja.” Maswahabah wakauliza: “Ni ipi hilo, ee Mtume wa Allaah?” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Ni lile litalokuwa katika yale niliyomo mimi hii leo na Maswahabah zangu.”

Tovuti hii iko na mafungamano ya karibu na wanachuoni. Bi maana pale kunapotokea majanga katika jamii, mambo makubwa yanayohusiana na ummah na mengineyo mfano wa hayo basi yanapelekwa kwa wanachuoni na wanatupatia ufumbuzi juu yake.

Tovuti hii ni yenye kujitegemea na binafsi na haisimamiwi na shirika, kampuni wala idara yoyote ile. Bali ni yenye kujitegemea na ni yenye kusimamia kazi zinazohusiana na wanachuoni kwa njia ya mwendelezo kwa kushirikiana na Firqatunnajia.com