Kipara Nje Ya ´Umrah Na Hajj

Swali: Je, kunyoa nywele (kupiga kipara) ni ´Ibaadah nje ya Hajj na ´Umrah? ´Allaamah al-Fawzaan: Hapana! Haijuzu kufanya hivi. Haijuzu kupiga kipara isipokuwa katika Hajj na ´Umrah. Hii ni Bid´ah (mtu akifanya hivi kwa kuamini ni ´Ibaadah) nje ya Hajj na ´Umrah. Na akinyoa kwa ajili ya kaburi la walii fulani na mfano wa hayo inakuwa ni Shirki kubwa. Swali La Pili: Je, ni katika alama za Khawaarij? ´Allaamah al-Fawzaan: Ndio. Ni katika alama za Khawaarij ikiwa ataweka ´Siymah` na akaweka alama, itakuwa ni katika alama za Khawaarij. Ama ikiwa hatoweka 'Siymah' wala alama, mtu akanyoa (akapiga kipara) kwa haja fulani, hakuna ubaya kufanya hivyo. Ama akanyoa kwa ajili zinakuwa ndefu sana, hakuna ubaya. Ama kukiwa ´Siymah` na alama, haya ni madhehebu ya Khawaarij.

Swali:
Je, kunyoa nywele (kupiga kipara) ni ´Ibaadah nje ya Hajj na ´Umrah?

´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana! Haijuzu kufanya hivi. Haijuzu kupiga kipara isipokuwa katika Hajj na ´Umrah. Hii ni Bid´ah (mtu akifanya hivi kwa kuamini ni ´Ibaadah) nje ya Hajj na ´Umrah. Na akinyoa kwa ajili ya kaburi la walii fulani na mfano wa hayo inakuwa ni Shirki kubwa.

Swali La Pili:
Je, ni katika alama za Khawaarij?

´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio. Ni katika alama za Khawaarij ikiwa ataweka ´Siymah` na akaweka alama, itakuwa ni katika alama za Khawaarij. Ama ikiwa hatoweka ‘Siymah’ wala alama, mtu akanyoa (akapiga kipara) kwa haja fulani, hakuna ubaya kufanya hivyo. Ama akanyoa kwa ajili zinakuwa ndefu sana, hakuna ubaya. Ama kukiwa ´Siymah` na alama, haya ni madhehebu ya Khawaarij.