Kila Usichokijua Wapinga?!

Kauli ya mwandishi (Rahimahu Allaah) - Imaam Abu Bakr - : “Wala usimpinge kwa ujinga”, yaani kitu usichokijua usikipinge. Sio kila kitu usichokijua unakipinga, bali unatakiwa kuamini yaliyo ya sahihi na kuthibiti hata kama hukijui (kitu hicho) na kukidiriki. Anasema (Ta´ala): بَلْ كَذَّبُوا بِمَا لَمْ يُحِيطُوا بِعِلْمِهِ وَلَمَّا يَأْتِهِمْ تَأْوِيلُهُ ۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ “Bali wamekadhibisha yale wasiyoyaelewa vyema elimu yake, na wala taawiyl (uhakika wake halisi) haujawafikia. Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale wa kabla yao.” (Yuunus:39) Wajibu ni Muislamu aamini yaliyothibiti kutoka kwa Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hata kama hakuyajua na hayakumwingia akilini, hili katika Mustaqbal litatokea: لِّكُلِّ نَبَإٍ مُّسْتَقَرٌّ ۚ وَسَوْفَ تَعْلَمُونَ “Kwa kila habari ina wakati (wake) maalumu, na mtakuja kujua.” (al-An´aam:67) Simulizi na khabari ambazo wameelezwa, kila kitu kina wakati wake. Itapokuja wakati wake kitadhihiri. Wajibu wetu ni kuamini. Kwa kuwa ni Maneno ya Allaah (Jalla wa ´Alaa): لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ “Haitokifikia ubatili mbele yake, na wala nyuma yake.” (Fuswswilat:42) Vilevile na maneno ya Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye hatamki kwa matamanio yake: وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ “Na wala hatamki kwa matamanio (yake). Hayo (ayasemayo) si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa (kwake).” (an-Najm:03-04) Haitakiwi kutegemea akili yetu, bali tuamini mambo ya ghaibu juu ya Wahyi uloteremka na tusiingize akili zetu na fikira zetu. Mambo ya ndani ya kaburi ni katika mambo ya Aakhirah, hata kama mtu atafunuliwa baada ya kumtia ndani ya kaburi lake tutamkuta vilevile kama tulivyomzika. Hata hivyo ameshakuwa katika ulimwengu mwingine na yanayompitikia hatuyaoni na wala hatuyahisi. Kwa kuwa yuko katika ulimwengu mwingine na amefichikana na sisi. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 162

Kauli ya mwandishi (Rahimahu Allaah) – Imaam Abu Bakr – : “Wala usimpinge kwa ujinga”, yaani kitu usichokijua usikipinge. Sio kila kitu usichokijua unakipinga, bali unatakiwa kuamini yaliyo ya sahihi na kuthibiti hata kama hukijui (kitu hicho) na kukidiriki. Anasema (Ta´ala):

بَلْ كَذَّبُوا بِمَا لَمْ يُحِيطُوا بِعِلْمِهِ وَلَمَّا يَأْتِهِمْ تَأْوِيلُهُ ۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ
“Bali wamekadhibisha yale wasiyoyaelewa vyema elimu yake, na wala taawiyl (uhakika wake halisi) haujawafikia. Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale wa kabla yao.” (Yuunus:39)

Wajibu ni Muislamu aamini yaliyothibiti kutoka kwa Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hata kama hakuyajua na hayakumwingia akilini, hili katika Mustaqbal litatokea:

لِّكُلِّ نَبَإٍ مُّسْتَقَرٌّ ۚ وَسَوْفَ تَعْلَمُونَ
“Kwa kila habari ina wakati (wake) maalumu, na mtakuja kujua.” (al-An´aam:67)

Simulizi na khabari ambazo wameelezwa, kila kitu kina wakati wake. Itapokuja wakati wake kitadhihiri. Wajibu wetu ni kuamini. Kwa kuwa ni Maneno ya Allaah (Jalla wa ´Alaa):

لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ
“Haitokifikia ubatili mbele yake, na wala nyuma yake.” (Fuswswilat:42)

Vilevile na maneno ya Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye hatamki kwa matamanio yake:

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ
“Na wala hatamki kwa matamanio (yake). Hayo (ayasemayo) si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa (kwake).” (an-Najm:03-04)

Haitakiwi kutegemea akili yetu, bali tuamini mambo ya ghaibu juu ya Wahyi uloteremka na tusiingize akili zetu na fikira zetu. Mambo ya ndani ya kaburi ni katika mambo ya Aakhirah, hata kama mtu atafunuliwa baada ya kumtia ndani ya kaburi lake tutamkuta vilevile kama tulivyomzika. Hata hivyo ameshakuwa katika ulimwengu mwingine na yanayompitikia hatuyaoni na wala hatuyahisi. Kwa kuwa yuko katika ulimwengu mwingine na amefichikana na sisi.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 162


  • Kitengo: Uncategorized , Barzakh (Maisha ya kaburini)
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 21st, February 2014