Khawaarij Hawaelewi Manufaa Yanayopatikana Kwa Kuwatii Watawala

Allaah (Ta´ala) amesema: يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا “Enyi mlioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo ni njia bora na matokeo mazuri zaidi.” (04:59) Kuwatii – watawala – ni katika kumtii Allaah. Mtawala akiamrisha kumtii Allaah (Tabaarak wa Ta´ala), akaamrisha jambo linaloruhusu [mubaah] midhali sio maasi, ni lazima kwa waumini kumsikiliza na kumtii ili kuhakikisha amri ya Allaah na Mtume Wake. Watekeleze hilo kwa kuchunga maslahi ya viumbe, Ummah na kuihifadhi Dini. Khawaarij hawajui mambo haya na hawayaelewi. Kwa ajili hii ndio maana harakati na mienendo yao inasababisha nyuma yake katika Ummah ufisadi na madhara yasiyojua yeyote isipokuwa Allaah katika kumgwada damu, ukiukwaji wa heshima [za watu], watu kuporwa, nafsi za watu zinakuwa na khofu na woga, ufisadi wa mauaji, wizi, uporaji unaenea na mengineyo. Kutokana na maslahi haya makubwa ambayo Khawaarij na wafuasi wao hawayatambui ndio maana Allaah na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakaamrisha kuwatii watawala. Mwandishi: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy Chanzo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaasid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/223) Toleo la: 17.04.2015 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا
“Enyi mlioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo ni njia bora na matokeo mazuri zaidi.” (04:59)

Kuwatii – watawala – ni katika kumtii Allaah. Mtawala akiamrisha kumtii Allaah (Tabaarak wa Ta´ala), akaamrisha jambo linaloruhusu [mubaah] midhali sio maasi, ni lazima kwa waumini kumsikiliza na kumtii ili kuhakikisha amri ya Allaah na Mtume Wake. Watekeleze hilo kwa kuchunga maslahi ya viumbe, Ummah na kuihifadhi Dini.

Khawaarij hawajui mambo haya na hawayaelewi. Kwa ajili hii ndio maana harakati na mienendo yao inasababisha nyuma yake katika Ummah ufisadi na madhara yasiyojua yeyote isipokuwa Allaah katika kumgwada damu, ukiukwaji wa heshima [za watu], watu kuporwa, nafsi za watu zinakuwa na khofu na woga, ufisadi wa mauaji, wizi, uporaji unaenea na mengineyo. Kutokana na maslahi haya makubwa ambayo Khawaarij na wafuasi wao hawayatambui ndio maana Allaah na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakaamrisha kuwatii watawala.

Mwandishi: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Chanzo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaasid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/223)
Toleo la: 17.04.2015
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Khawaarij
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 17th, April 2015