Kajitahidi Kukiafiki Qiblah Lakini Kapinda Kidogo

Muulizaji: Mtu akiswali katika bara na hakujitahidi kukielekea Qiblah, lakini hata hivyo kapinda kidogo tu. Imaam Ibn Baaz: Ikiwa hakujitahidi (kukitafuta Qiblah) atarudi kuswali upya. Muulizaji: Lakini kakiafiki Qiblah bila ijitihadi yoyote. Imaam Ibn Baaz: Ikiwa kakiafiki Qiblah sawa. Muulizaji: Hata kama hakujitahidi? Imaam Ibn Baaz: Hata kama, maadamu tu kaswali akiitakidi hichi ndo Qiblah Alhamduli Allaah, hili ndo linalohitajika. Maadamu kaswali akiitakidi hichi ndo Qiblah, Alhamduli Allaah. Muulizaji: Vipi ikiwa yuko mjini? Imaam Ibn Baaz: Hapana haitosihi, kwa kuwa mjini ni tofauti. Itabidi alipe [Swalah hio]. Kwa kuwa akiwa mjini anaweza kumuuliza mtu Qiblah kilipo na kuna Misikiti.

Muulizaji:
Mtu akiswali katika bara na hakujitahidi kukielekea Qiblah, lakini hata hivyo kapinda kidogo tu.

Imaam Ibn Baaz:
Ikiwa hakujitahidi (kukitafuta Qiblah) atarudi kuswali upya.

Muulizaji:
Lakini kakiafiki Qiblah bila ijitihadi yoyote.

Imaam Ibn Baaz:
Ikiwa kakiafiki Qiblah sawa.

Muulizaji:
Hata kama hakujitahidi?

Imaam Ibn Baaz:
Hata kama, maadamu tu kaswali akiitakidi hichi ndo Qiblah Alhamduli Allaah, hili ndo linalohitajika. Maadamu kaswali akiitakidi hichi ndo Qiblah, Alhamduli Allaah.

Muulizaji:
Vipi ikiwa yuko mjini?

Imaam Ibn Baaz:
Hapana haitosihi, kwa kuwa mjini ni tofauti. Itabidi alipe [Swalah hio]. Kwa kuwa akiwa mjini anaweza kumuuliza mtu Qiblah kilipo na kuna Misikiti.