Jukumu Kubwa Lililo Juu Ya Wanafunzi

´Allaamah Muhammad al-Jaamiy: Kumfunza mjinga ni wajibu hata kama hakukuomba huyu mjinga. Kwa kuwa kuna aina mbili za kuomba; kuna kuomba kwa [ulimi] kwa njia ya mtu kukutamkia na kuna kuomba kwa njia ya [kuiona] hali ya mtu. Bi maana, umemuona mtu anaswali hovyo hovyo Swalah yake, hatimizi Rukuu, Sujuud. Kaswali faradhi na wewe umemuona, hana utulivu. Kaswali kimakosa. Lau utamwacha utakuwa umefanya makosa. Kwa kuwa amekuomba kwa njia ya hali yake, kutokana na haya makosa ya Swalah yake kakuomba kwa njia ya hali yake kwa kuwa hajui. Usisubirie kutoka kwake ya kuwa atakujia na kukuuliza. Vipi atakuuliza naye ni mjinga asiyejijua? Hajui na hajui kama hajui. Hivyo ni wajibu kumnasihi. Dalili ya hilo ni kisa cha yule aliyeswali kimakosa. Mtu ambaye aliingia Msikiti huu [al-Masjid an-Nabawiy] akaswali Rakaa mbili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anamtazama, akamuacha, akaswali na kumaliza kisha akamjia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumtolea Salaam na Mtume akamrudishia Salaam. Akamwambia: "Rejea ukaswali tena, kwani kwa hakika hukuswali." Tazama ibara hii: "... kwani kwa hakika hukuswali." Swalah ambayo hakuiswali kwa utulivu si Swalah, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kaita kuwa si Swalah. "Rejea ukaswali tena, kwani kwa hakika hukuswali." Akarudia kuswali kama alivyoswali mara ya kwanza, akarejea na kumsalimia Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) na akamrudishia Salaam. Akamwambia: "Rejea ukaswali tena, kwani kwa hakika hukuswali." Akashangaa. Akarudia na kuswali kama alivyoswali kabla yake, akafanya hivyo mara tatu. Mtu yule alichoka, mara ya tatu akasema: "Naapa kwa yule Aliyekutuma kwa haki, siwezi kufanya bora zaidi ya hapa." Amekubali ujinga wake. Na alikuwa akidhani kuwa ndio Swalah sahihi. Kwa ajili hiyo, tutapomuona mtu anayedokoea katika Swalah yake - kama mtu yule - ni wajibu kwetu kumnasihi na kumtanabahisha. Kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), hata kama hakukuomba kwa njia ya kutamka, kwa kuwa kishakuomba kwa njia ya hali yake. Hii Hadiyth kubwa, tunapata mafunzo ya kwamba kutengeneza, kuamrisha mame na kuondoshamaovu, na Bid´ah ikiwa uko na elimu basi ni wajibu kwako hata kama hukuombwa. Hivyo, watafutaji wa elimu [wanafunzi] wana jukumu kubwa kabisa na hususan katika wakati huu na jamii tunazoishi ndani yake. Na wametapakaa Waislamu duniani kote. Kuko [katika Waislamu] ambao hawajui katika Uislamu lolote zaidi ya kule kujinasibisha tu, hajui vipi kuswali, nyie mnaona wanavyodokoa katika Swalah zao na wanavyozusha. Imamu anaswali faradhi anakuja mtu na kuswali Swalah ya Nawaafil. Wanaswali Nawaafil huku Imamu anaswali Swalah ya faradhi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kakataza hilo. Ndugu yako Muislamu ambaye ana ujinga kama huu, basi ni wajibu juu yako kumfunza na usisubirie kutoka kwake aanze kukuomba. Yule atakayekuuliza ni yule ambaye kajua ya kwamba hajui, na ujinga umeenea leo kati ya safu za Waislamu wengi wa leo wana ujinga wa kutojijua. Ikiwa hujui ya kwamba hujui, basi huyo ni ujinga juu ya ujinga. Ujinga aina mbili. Ni wajibu kutanabahisha.

´Allaamah Muhammad al-Jaamiy:

Kumfunza mjinga ni wajibu hata kama hakukuomba huyu mjinga. Kwa kuwa kuna aina mbili za kuomba; kuna kuomba kwa [ulimi] kwa njia ya mtu kukutamkia na kuna kuomba kwa njia ya [kuiona] hali ya mtu. Bi maana, umemuona mtu anaswali hovyo hovyo Swalah yake, hatimizi Rukuu, Sujuud. Kaswali faradhi na wewe umemuona, hana utulivu. Kaswali kimakosa. Lau utamwacha utakuwa umefanya makosa. Kwa kuwa amekuomba kwa njia ya hali yake, kutokana na haya makosa ya Swalah yake kakuomba kwa njia ya hali yake kwa kuwa hajui. Usisubirie kutoka kwake ya kuwa atakujia na kukuuliza. Vipi atakuuliza naye ni mjinga asiyejijua? Hajui na hajui kama hajui. Hivyo ni wajibu kumnasihi. Dalili ya hilo ni kisa cha yule aliyeswali kimakosa. Mtu ambaye aliingia Msikiti huu [al-Masjid an-Nabawiy] akaswali Rakaa mbili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anamtazama, akamuacha, akaswali na kumaliza kisha akamjia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumtolea Salaam na Mtume akamrudishia Salaam. Akamwambia: “Rejea ukaswali tena, kwani kwa hakika hukuswali.”

Tazama ibara hii: “… kwani kwa hakika hukuswali.” Swalah ambayo hakuiswali kwa utulivu si Swalah, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kaita kuwa si Swalah. “Rejea ukaswali tena, kwani kwa hakika hukuswali.”
Akarudia kuswali kama alivyoswali mara ya kwanza, akarejea na kumsalimia Mtume (Swalla Allaahu´alayhi wa sallam) na akamrudishia Salaam. Akamwambia: “Rejea ukaswali tena, kwani kwa hakika hukuswali.” Akashangaa. Akarudia na kuswali kama alivyoswali kabla yake, akafanya hivyo mara tatu.
Mtu yule alichoka, mara ya tatu akasema: “Naapa kwa yule Aliyekutuma kwa haki, siwezi kufanya bora zaidi ya hapa.” Amekubali ujinga wake. Na alikuwa akidhani kuwa ndio Swalah sahihi. Kwa ajili hiyo, tutapomuona mtu anayedokoea katika Swalah yake – kama mtu yule – ni wajibu kwetu kumnasihi na kumtanabahisha. Kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), hata kama hakukuomba kwa njia ya kutamka, kwa kuwa kishakuomba kwa njia ya hali yake. Hii Hadiyth kubwa, tunapata mafunzo ya kwamba kutengeneza, kuamrisha mame na kuondoshamaovu, na Bid´ah ikiwa uko na elimu basi ni wajibu kwako hata kama hukuombwa.
Hivyo, watafutaji wa elimu [wanafunzi] wana jukumu kubwa kabisa na hususan katika wakati huu na jamii tunazoishi ndani yake. Na wametapakaa Waislamu duniani kote. Kuko [katika Waislamu] ambao hawajui katika Uislamu lolote zaidi ya kule kujinasibisha tu, hajui vipi kuswali, nyie mnaona wanavyodokoa katika Swalah zao na wanavyozusha. Imamu anaswali faradhi anakuja mtu na kuswali Swalah ya Nawaafil. Wanaswali Nawaafil huku Imamu anaswali Swalah ya faradhi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kakataza hilo. Ndugu yako Muislamu ambaye ana ujinga kama huu, basi ni wajibu juu yako kumfunza na usisubirie kutoka kwake aanze kukuomba. Yule atakayekuuliza ni yule ambaye kajua ya kwamba hajui, na ujinga umeenea leo kati ya safu za Waislamu wengi wa leo wana ujinga wa kutojijua. Ikiwa hujui ya kwamba hujui, basi huyo ni ujinga juu ya ujinga. Ujinga aina mbili. Ni wajibu kutanabahisha.