Je, Wewe Ni Katika Kikundi Kilichookoka?

´Allaamah al-Jaamiy: Kasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "[Makundi] Yote yataingia Motoni isipokuwa kundi limoja tu." Maswahabah wakauliza: "Ni lipi hilo ewe Mtume wa Allaah?" Akasema: "Ni lile litalokuwa katika yale niliyomo leo mimi na Maswahabah wangu." Yaani wale wasiyobadilisha, hawazidisha wala hawapunguzi. Wamekoma katika yale aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah. Njia ya dhahiri iliyonyooka. Mfumo mweupe kabisa aliyoashiria Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwisho wa maisha yake. Alipowaambia Maswahabah wake: "Nimewaacha katika njia nyeupe usiku wake ni sawa na mchana wake, hatopotea humo ila mpotofu.” Huwezi kujua kuwa wewe uko katika yale aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaah ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake? Na je wewe uko katika yale waliyokuwemo Jamaa´ah? Kwa kuwa baadhi ya Riwaayah imekuja Jamaa´ah. Kipote kitachookoka ni Jamaa´ah. Lakini utajuaje kikundi hicho [kwa kuwa] makundi ni mengi. Ni lazima kuwa na ufahamu katika Dini [kusoma]. La sivyo, kila mmoja anadai kwa kujinasibisha na Layla na Layla yuko mbali na wote hao. Kila mmoja anadai mimi ni katika kipote kilichookoka. [wanasema] sisi ni katika makundi ya Kiislamu na "sisi" na "sisi" na "sisi." Da´wah zipo nyingi. Ila utajuaje? Kwa kuwa na ufahamu katika Dini. Jua aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika ´Aqiydah yako, jua ´Aqiydah ya Maswahabah. Walikuweje katika ´Ibaadah zao? Walikuweje katika tabia zao? Walikuweje katika kuamiliana kwao [na watu] na mambo mengine yote?

´Allaamah al-Jaamiy:

Kasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“[Makundi] Yote yataingia Motoni isipokuwa kundi limoja tu.” Maswahabah wakauliza: “Ni lipi hilo ewe Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni lile litalokuwa katika yale niliyomo leo mimi na Maswahabah wangu.”

Yaani wale wasiyobadilisha, hawazidisha wala hawapunguzi. Wamekoma katika yale aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah. Njia ya dhahiri iliyonyooka. Mfumo mweupe kabisa aliyoashiria Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwisho wa maisha yake. Alipowaambia Maswahabah wake:

“Nimewaacha katika njia nyeupe usiku wake ni sawa na mchana wake, hatopotea humo ila mpotofu.”
Huwezi kujua kuwa wewe uko katika yale aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaah ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake? Na je wewe uko katika yale waliyokuwemo Jamaa´ah? Kwa kuwa baadhi ya Riwaayah imekuja Jamaa´ah. Kipote kitachookoka ni Jamaa´ah. Lakini utajuaje kikundi hicho [kwa kuwa] makundi ni mengi. Ni lazima kuwa na ufahamu katika Dini [kusoma]. La sivyo, kila mmoja anadai kwa kujinasibisha na Layla na Layla yuko mbali na wote hao. Kila mmoja anadai mimi ni katika kipote kilichookoka. [wanasema] sisi ni katika makundi ya Kiislamu na “sisi” na “sisi” na “sisi.”

Da´wah zipo nyingi. Ila utajuaje? Kwa kuwa na ufahamu katika Dini. Jua aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika ´Aqiydah yako, jua ´Aqiydah ya Maswahabah. Walikuweje katika ´Ibaadah zao? Walikuweje katika tabia zao? Walikuweje katika kuamiliana kwao [na watu] na mambo mengine yote?