Wakristo Wa Leo Wanatakiwa Kuitwa Makafiri Wa Kinaswara

Swali:
Katika darsa iliyopita ulisema kuwa mtu asisemi "Masihiyyuun" na badala yake mtu aseme "Manaswara"...

Jibu:

Ndio, hili ndio linalopatikana katika Qur-aan. Masihiyyuun maana yake ni kwamba wanamfuata al-Masiyh hivi sasa. Pamoja na kuwa wao sio wafuasi wa al-Masiyh (´alayhis-Swalaatu was-Salaam). Baada ya kutumwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakamkanusha hawazingatiwi kuwa ni wafuasi wa al-Masiyh hata kama watajinasibisha naye. Wao ni makafiri. Kwa kuwa wamemkufuru al-Masiyh na wamewakufuru Mitume wote. Kumkufuru kwao Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kuwakufuru Mitume wote. Kwa hivyo wao sio Masihiyyuun. Hili ni mosi.

Pili ni kuwa wanasema kuwa Allaah ni utatu na kwamba Allaah ni al-Masiyh mwana wa Maryam. Je, mtu atasema kuwa watu hawa ni Masihiyyuun? Hawa ni makafiri. Ni makafri wa kinaswara. Hawa ni makafiri wa kinaswara:

لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ
“Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni watatu wa utatu.”” (05:73)

لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ
“Kwa yakini, wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah Ndiye al-Masiyh mwana wa Maryam.” Sema: “Nani anayemiliki chochote mbele ya Allaah akitaka kumhilikisha al-Masiyh mwana wa Maryam.”” (05:17)

Wao ni makafiri wa kinaswara.

Hata kuwaita neno hili la manaswara ni [sauti haiko wazi]. Wanatakiwa kuitwa makafiri wa kinaswara.

Mzungumzaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (22) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2134
Toleo la: 09.01.2016
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: , Wakristo na ukristo
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 9th, January 2016