Vitu Vya Duniani Vinafanana Na Vya Aakhirah Kwa Njia Ya Majina Tu

Swali:
Matunda ya duniani ni kama matunda ya Aakhirah katika sifa, aina na ladha yake?

Jibu:

Ni mfano wake kwa njia ya jina tu. Mkomamanga wa hapa duniani na wa Peponi unaitwa vivyo hivyo. Mitende ya hapa duniani na ya Peponi inaitwa vivyo hivyo. Majina yanashirikiana lakini uhakika wake vinatofautiana. Hali kadhalika maziwa, maji, pombe, asajali n.k. vinatofautiana katika uhakika wake na ni vyenye kufanana katika majina. Kwa ajili hii Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Vilivyopo Peponi miongoni mwa vitu vilivyopo duniani ni kwa majina tu.”

Hili ni kwa mikomamanga, mitende, matunda na kadhalika.

Mzungumzaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (17) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-11-6.mp3
Toleo la: 20-02-2015
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: , Pepo
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 20th, February 2015