Vipi Muislamu Ataweza Kuisahihisha ´Aqiydah Yake?

Swali:
Vipi Muislamu ataisahihisha ´Aqiydah yake ya Kiislamu na vipi ataihifadhi ´Aqiydah yake?

Jibu:

Awe na ufahamu katika Dini. Asome na kujifunza mpaka aweze kuijua ´Aqiydah na kuihifadhi. Awaulize wanachuoni na ikiwa ni mwanafunzi aizingatie Qur-aan na Sunnah mpaka aijue ´Aqiydah sahihi ambayo inatolewa dalili na Qur-aan na ashikamane nayo na awe na Istiqaamah juu yake. Na ikiwa anatatizika, awaulize wanachuoni ambao anawaamini juu ya yale ambayo yanamtatiza mpaka awe juu ya Baswiyrah.


  • Author: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • http://binbaz.org.sa/mat/10261
  • Kitengo: , ´Aqiydah
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Wednesday 8th, January 2014