Qur-aan Ni Katika Sifa Za Allaah

Swali:
Watu wa batili wanatumia dalili kwa Aayah hii ifuatayo. Amesema (Ta´ala): اللَّـهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ "Allaah ndiye Muumbaji wa kila kitu." (39:62) Wanasema kuwa Qur-aan inaingia katika jumla ya vitu. Vipi tutawaraddi?

Jibu:

Qur-aan ni miongoni mwa Sifa za Allaah ambapo haingii miongoni mwa vitu vilivyoumbwa. Qur-aan ni Sifa miongoni mwa Sifa za Allaah, haingii katika vitu vilivyoumbwa. Sifa Zake haziingii katika vitu vilivyoumbwa. Allaah kwa Sifa Zake ni Muumbaji na visivyokuwa hivyo vimeumbwa. Vinginevyo tunaweza kusema kuwa Allaah pia ameumbwa kwa sababu Yeye ni kitu. Ni nani mwenye kusema hivo? Haijuzu kusema hivo.

Mzungumzaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (4) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir–14331228.mp3
Toleo la: 17.06.2015
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: , Maneno ya Allaah
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Wednesday 17th, June 2015