Nasaha Tatu Tosha Kwa Anayewatukana Wanachuoni

Swali:
Kuna kijana anayewatukana baadhi ya wanachuoni. Hata hivyo kuna baadhi ya vijana wa ki-Salafiy wanaotangamana naye. Baadhi yao wanatumia hoja kuwa wanamnasihi na wengine wanatumia moja kuwa wanakaa naye kwa ajili ya mambo ya kidunia. Ni ipi hukumu ya watu hawa?

Jibu:

Ikiwa wanakaa naye kwa ajili ya kumpa nasaha, nasaha inachukua kikao kimoja, viwili au vitatu. Ama kukaa nae kila siku na kusema kuwa mnamnasihi si sawa.