Mume Kunyonya Matiti Ya Mke Wake

Swali:
Je, mke huwa haramu kwa mume wake akinyonya matiti yake mara nne?

Jibu:

Allaah Kamhalalishia mume kufurahi kwa mkewe atakavyo. Anaweza hata kufanya naye mapenzi kwa njia mbalimbali. Allaah (Ta´ala) Kasema:

نسآؤكم حرث لكم فأتوا حرثكم أنى شئتم
“Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu vyovyote mpendavyo.” (al-Baqarah 02 :223)

Zingatia kauli “basi ziendeeni konde zenu vyovyote mpendavyo.” Konde ni mahali pa rutuba ambapo ni tupu ya mwanamke. Hivyo ni halali kwa mume kufanya kitendo cha ndoa kwenye tupu ya mke sawa ikifanywa kwa mbele, kwa nyuma, kwa kusimama, kwa kulala au kupitia nafasi nyingine yoyote kwa sharti iwe ni kwenye tupu yake ya mbele. Hali kadhalika, anaweza kufurahi naye kwa kumkumbatia, kumkisi na kumbusu vile apendavyo. Kilichoharamishwa tu ni yeye [mume] kufanya naye kitendo cha ndoa wakati wa hedhi na liwati [nyuma].

Kulingana na kanuni hii ya jumla, anaweza kunyonya maziwa ya mkewe. Hawi [mke] haramu kwake [mume] hata kama lau atakunywa maziwa yake. Haya ndio maoni ya jamhuri. Ili kunyonyesha kuathiri ni lazima mtu awe chini ya miaka miwili. Baada ya hapo hakuathiri kitu chochote. Hali kadhalika ni lazima kunyonyesha kufanyike angalau mara tano ili kuharamike. Vinginevyo hakuathiri chochote.


  • Author: Imaam Muhammad bin Swaalih bin 'Uthaymiyn. Nuur 'alaad-Darb (16A)
  • Kitengo: , Kujamiiana
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Wednesday 11th, December 2013