Mtume Haombwi Uombezi Baada Ya Kufa

Swali:
Ni ipi hukumu ya mwenye kuomba uombezi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada kufa kwake?

Jibu:

Maiti haiobwi kitu, sawa ikiwa ni uombezi au kitu kingine.[1] Maswahabah hawakuwa wanaenda kwenye kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumuomba Du´aa, uombezi au Istighfaar. Wao ni wajuzi zaidi katika Ummah juu ya yanayojuzu na yasiyojuzu kwa kuwa wao ni wanafunzi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lau wangelijua kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa jambo hili linajuzu wangelifanya. Kile kitendo chao cha wao kuacha ni kwamba walijua kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa kitendo hichi hakijuzu na hakifanywi.

——
(1) Tazama http://www.wanachuoni.com/content/kumuomba-maiti-msamaha-baada-ya-kufa

Mzungumzaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-1-30.mp3
Toleo la: 9-02-2015
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: , Aakhirah
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Monday 9th, February 2015