Mtu Ananufaika Baada Ya Kufa Kwa Vitabu Alivyoeneza?

Swali:
Nikinunua misahafu, vijitabu, vipeperushi au vitabu vya elimu na nikavitawanya inaingia katika Hadiyth isemayo: "Anapofariki mwanaadamu hukatika matendo yake isipokuwa vitu vitatu; swadaqah yenye kuendea, elimu yenye kunufaika kwayo au mtoto mwema mwenye kumuombea"?

Jibu:

Ndio, vinaingia humo. Ukinunua vitabu vyenye manufaa na ukavitawanya inaingia katika elimu yenye kunufaika kwayo.

Mzungumzaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: Sharh Fath-il-Majiyd (35) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majid%20-%208%20-…
Toleo la: 07.05.2016
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: , Yanayomnufaisha maiti baada ya kufa
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 7th, May 2016