Mali Ya Mke Anayomuazima Mume Wake

Swali:
Nilimnunulia mke wangu dhahabu. Wakati nilipohitajia kiwango cha pesa akaniuzia kwa ridhaa yake na nikatumia mali hiyo. Je, ni lazima kwangu kumrudishia wakati atakaponiomba hilo?

Jibu:

Ikiwa ameikupa na akakuruhusu [kuitumia], sio wajibu kumrudishia. Ama ikiwa ameikupa kwa sharti umrudishie nayo [baadaye] au umrudishie kiwango badala yake, ni wajibu kumrudishie. Isipokuwa tu ikiwa kama atakusamehe.