Kuweka Qur-aan Ndani Ya Gari Kama Ulinzi

Swali:
Inazingatiwa kuwa ni kutafuta ulinzi kwa maneno ya Allaah kuweka msahafu ndani ya gari ili uilinde gari dhidi ya shari?

Jibu:

Hapana. Huku ni kuweka hirizi. Haijuzu. Msahafu hautumiwi kama hirizi. Msahafu unatumiwa kwa ajili ya kusoma na kudurusu. Haijuzu kuutumia kwa ajili ukuhifadhi wewe mwenyewe, gari yako au nyumba yako.

Mzungumzaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: Sharh Fath-il-Majiyd (36) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majd%20-%2030%20-%2012%20-%201436.mp3
Toleo la: 09.05.2016
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: , Imani, Kufuru na Shirki
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Monday 9th, May 2016