Kusema Mtume Wetu Fulani Mbali Na Mtume Wetu Muhammad (´alayhis-Salaam)

Swali:
Je, ni sahihi ya kwamba haijuzu kwetu kusema kuhusiana na Muusa (´alayhis-Salaam) tukasema "Mtume wetu Muusa", na "Mtume wetu ´Iysa." Kwa kuwa Mtume wetu sisi ni Muhammad (´alayhis-Salaam), bali anapotajwa yatakikana kusema "Mtume wa Allaah Muusa"?

Jibu:

Ndio, ni kweli. Mtu anatakikana kusema “Mtume wa Allaah Muusa”. Vile vile ni Mtume wa Bani Israaiyl. Mtume wetu ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).