Kukusanyika Kusoma Qur-aan Kwa Ajili Ya Kupata Baraka Kazini

Swali:
Je, inajuzu kwa mtu kuwakusanya watu na akawaamrisha kumsomea Qur-aan kwa lengo moja wapo kama mfano wa kubadilisha kazi na akawakusanya watu wamsomee Qur-aan ili aweze kufikiwa na baraka katika kazi yake?

Jibu:

Allaah ameteremsha Qur-aan ili watu waabudu kwa kisomo chake na kutendea kazi hukumu zake na iwe ni miujiza kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kitendo hichi ulichotaja sio miongoni mwa mambo yaliyoweka Allaah (Subhaanah).

Mwandishi: al-Lajnah ad-Daaimah
Chanzo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (343/02)
Toleo la: 09.09.2015
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: , Kutabaruku
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Wednesday 9th, September 2015