Je, Watoto Wa Makafiri Ni Katika Ahl-ul-Fatrah?

Swali:
Je, watoto wa washirikina wanachukuliwa ni katika Ahl-ul-Fatrah?

Jibu:

Wametofautiana wanachuoni kuhusu wao. Suala lao liko kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Hukmu yao duniani, wanawafuata baba zao. Wanafanyiwa yanayofanyiwa makafiri. Ama Aakhirah, suala lao liko kwa Allaah.