Ipi Bora; Kumuomba Mtu Aniombee Du´aa Au Kujiombea Mwenyewe?

Swali:
Je, ni bora kwa mtu kujiombea Du´aa mwenyewe au aombe Du´aa kutoka kwa mtu asiyekuwepo?

Jibu:

Hapana, bora ni yeye kujiombea mwenyewe. Kwa kuwa Du´aa ni ´Ibaadah. Kule kumuabudu Allaah kwa Du´aa ni bora kuliko kuwaendea wengine.Anasema pia Shaykh-ul-Islaam [Ibn Taymiyyah]:

“Kumuomba mtu mwengine akuombee Du´aa, kuna kuwahitajia viumbe na udhalili kwa viumbe.”

Jitajirishe kwa viumbe na muombe Allaah mwenyewe, hili ni aula zaidi na bora.