Hirizi Karibu Na Kichwa

Swali:
Kuna mtu siku zote kichwa chamuuma. Akaenda kwa tabibu ambaye alimpa kipande cha kitambaa kilichoshonwa na akamwambia akiweke chini ya kichwa chake wakati wa kulala. Pindi alipomuuliza kina nini, akamwambia kuwa kina Aayah za Qur-aan na du´aa za kinabii. Imewekwa katika Shari´ah kukitumia?

Jibu:

Hapana. Hii ni hirizi. Kabla ya kwenda kulala asome Qur-aan na Suurah “al-Ikhlaasw”, “al-Falaq” na “an-Naas” na Aayah al-Kursiy. Haya ndio yenye kumnufaisha. Kuweka hirizi karibu na kichwa chake haijuzu na wala haimnufaishi kitu.

Mzungumzaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: Sharh Fath-il-Majiyd (36) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majd%20-%2030%20-%2012%20-%201436.mp3
Toleo la: 09.05.2016
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: , Imani, Kufuru na Shirki
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Monday 9th, May 2016