Hadiyth al-Qudsiy Ni Maneno Ya Allaah

Swali:
Ipi kauli yenye nguvu kuhusiana na Hadiyth al-Qudsiy, je lafdhi na maana yake ni kutoka kwa Allaah au ni maana peke yake?

Jibu:

Kauli yenye nguvu ni kwamba lafdhi na maana yake ni kutoka kwa Allaah. Lakini inatofautiana na Qur-aan kwa kule mtu kutofanya nayo ´Ibaadah kwa kisomo chake. Hata hivyo, ni yenye kutoka kwa Allaah, ni kama Tawrat na Injiyl na kama jinsi Allaah Alivyomkhutubia Muusa na kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokwenda Mi´iraaj. Yote haya ni Maneno ya Allaah. Kwa kuwa Hadiyth al-Qudsiy anasema Mtume wa Allaah: “Allaah Kasema… “. Ingelikuwa maana tu ndio inatoka kwa Allaah na lafdhi ni ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), usahihi ingekuwa ni kusema: “Kasema Mtume wa Allaah… “. Bali Mtume wa Allaah kaipokea kutoka kwa Mola Wake (´Azza wa Jalla) na ndio maana anasema: “Kasema Allaah (´Azza wa Jalla)”.