al-Lajnah ad-Daaimah Kuhusu Kusoma Qur-aan Bila Wudhuu

Swali:
Je, inajuzu kwangu kusoma Qur-aan ikiwa sina janaba lakini hata hivyo sikutawadha? Je, inajuzu kusoma ilihali sikuelekea Qiblah?

Jibu:

Inajuzu kusoma Qur-aan kwa asiyekuwa na janaba hata kama hakutawadha na hakuelekea Qiblah. Lakini hata hivyo usiguse msahafu isipokuwa mpaka uwe uko na twahara kutokana na hadathi kubwa na ndogo.

Mwandishi: al-Lajnah ad-Daaimah
Chanzo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (78/04)
Toleo la: 23.09.2015
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: , Kuhusu kugusa Qur-aan katika wakati mtu hana twahara
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Wednesday 23rd, September 2015