Aidha Kusamehe Baadhi Ya Haki Zako Au Talaka

Swali:
Kuna mwanaume ameoa wake wawili. Kukatokea baina yake yeye na mmoja wao migogoro. Akampa khiyari ya mambo mawili, ima kuachana au abake pamoja naye lakini kwa sharti ya kusamehe baadhi ya wakati wake kumpa yule mke mwengine.

Jibu:

Hakuna neno katika hili. Hakuna neno akawaambia kwamba hawezi kufanya uadilifu baina yao, mkipenda mtabaki na mimi katika hali yangu hii na kama huwezi nakutaliki. Ana haki ya kufanya hivyo. Dalili ya hili ni kwamba Sawdah bint Zam´ah (Radhiya Allaahu ´anha) alikuwa ni mzee. Akakhofia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atamtaliki. Akamwambia:

“Ewe Mtume wa Allaah! Mimi nampa siku yangu ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha).”

Hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa analala kwa ´Aaishah siku mbili. Siku moja ilikuwa ya ´Aaishah na nyingine ilikuwa ni siku ya Sawdah na Sawdah akawa hakubaki na siku. Hakuna neno.


  • Author: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn. Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (13 B)
  • Kitengo: , Nafaqaat (Ugavi)
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 30th, March 2014