Hutoniona Kamwe Au Hutoniona?

Allaah (Subhaanah) Anasema: ولما جاء موسى لميقاتنا وكلمه ربه قال رب أرني أنظر إليك قال لن تراني "Na alipokuja Muwsaa katika miyqaat (pahala pa miadi) yetu, na Mola wake Akamsemesha, (Muwsaa) alisema: “Mola wangu! Nionyeshe ili nikutazame.” (Allaah) Akasema: “Hutoniona!"." Anaeleza (Ta´ala) kwamba baada ya Muusa ('alayhis-Salaam) kuja katika miadi ya Allaah (Ta´ala) na Akazungumza Naye (Ta´ala), akamuomba ajionyeshe kwake ili amtazame Yeye. Akasema: “Mola wangu! Nionyeshe ili nikutazame.” Wanachuoni wengi wametatizika kuhusiana na neno "Lan" na kuwa linamaanisha "kamwe" au hapana. Mu'tazilah wamelitumia kwa kuthibitisha kuwa Allaah hatoonekana si katika maisha haya wala maisha baada ya haya. Hata hivyo, haya ni maoni dhaifu. Kumepokelewa [mapokezi mengi] kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ya kwamba waumini watamuona Allaah siku ya Qiyaamah. Dalili nyingine ya hilo ni Kauli Yake Allaah kuhusu makafiri: كلا إنهم عن ربهم يومئذ لمحجوبون "Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa kumuona Mola Wao". Ili kuoanisha Aayah pamoja na Hadiyth zisemazo ya kwamba Allaah ataonekana siku ya Qiyaamah, baadhi yao wamesema kwamba "Lan" inamaanisha ya kwamba Allaah kamwe hatoonekana katika maisha haya [ya duniani]. Wengine wamesema maneno katika hali hii ni kama maneno katika Kauli Yake (Ta´ala): لا تدركه الأبصار وهو يدرك الأبصار وهو اللطيف الخبير "Macho hayamdiriki (hayamfikii) bali Yeye Anayadiriki macho; Naye Al-Latwiyful-Khabiyr (Mwenye Kudabiri mambo kwa utuvu, Mjuzi - Mjuzi wa undani na ukina wa mambo)." Maelezo yake yameshatajwa tayari katika Suurat "al-An'aam". Katika maandiko ya kale yasemekana ya kwamba Allaah (Ta´ala) alimwambia Muusa ('alayhis-Salaam): "Muusa! Hakuna mtu yeyote atakayeniona mpaka afe kwanza." Mwandishi: Imaam Isma´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy Chanzo: Tafsiyr al-Qur-aan al-'Adhwiym (2/325-326) Mu'assasah ar-Risaalah, 1422/2001

Allaah (Subhaanah) Anasema:

ولما جاء موسى لميقاتنا وكلمه ربه قال رب أرني أنظر إليك قال لن تراني
“Na alipokuja Muwsaa katika miyqaat (pahala pa miadi) yetu, na Mola wake Akamsemesha, (Muwsaa) alisema: “Mola wangu! Nionyeshe ili nikutazame.” (Allaah) Akasema: “Hutoniona!”.”

Anaeleza (Ta´ala) kwamba baada ya Muusa (‘alayhis-Salaam) kuja katika miadi ya Allaah (Ta´ala) na Akazungumza Naye (Ta´ala), akamuomba ajionyeshe kwake ili amtazame Yeye. Akasema:

“Mola wangu! Nionyeshe ili nikutazame.”

Wanachuoni wengi wametatizika kuhusiana na neno “Lan” na kuwa linamaanisha “kamwe” au hapana. Mu’tazilah wamelitumia kwa kuthibitisha kuwa Allaah hatoonekana si katika maisha haya wala maisha baada ya haya. Hata hivyo, haya ni maoni dhaifu. Kumepokelewa [mapokezi mengi] kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ya kwamba waumini watamuona Allaah siku ya Qiyaamah. Dalili nyingine ya hilo ni Kauli Yake Allaah kuhusu makafiri:

كلا إنهم عن ربهم يومئذ لمحجوبون
“Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa kumuona Mola Wao”.

Ili kuoanisha Aayah pamoja na Hadiyth zisemazo ya kwamba Allaah ataonekana siku ya Qiyaamah, baadhi yao wamesema kwamba “Lan” inamaanisha ya kwamba Allaah kamwe hatoonekana katika maisha haya [ya duniani].

Wengine wamesema maneno katika hali hii ni kama maneno katika Kauli Yake (Ta´ala):

لا تدركه الأبصار وهو يدرك الأبصار وهو اللطيف الخبير
“Macho hayamdiriki (hayamfikii) bali Yeye Anayadiriki macho; Naye Al-Latwiyful-Khabiyr (Mwenye Kudabiri mambo kwa utuvu, Mjuzi – Mjuzi wa undani na ukina wa mambo).”

Maelezo yake yameshatajwa tayari katika Suurat “al-An’aam”. Katika maandiko ya kale yasemekana ya kwamba Allaah (Ta´ala) alimwambia Muusa (‘alayhis-Salaam):

“Muusa! Hakuna mtu yeyote atakayeniona mpaka afe kwanza.”

Mwandishi: Imaam Isma´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
Chanzo: Tafsiyr al-Qur-aan al-‘Adhwiym (2/325-326)
Mu’assasah ar-Risaalah, 1422/2001


  • Kitengo: Uncategorized , Kuonekana kwa Allaah siku ya Qiyaamah
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013