Hawa Hapa Wanaume Wetu – Wako Wapi Wanaume Wenu? (2)

1) Sa´iyd bin ´Aamir adh-Dhab'iy (d. 208) - Imaam wa Basrah - kasema: "Jahmiyyah wana mtazamo mbaya zaidi kuliko Mayahudi na Wakristo. Dini zote ikiwa ni pamoja na Waislamu wamekubaliana ya kwamba Allaah Yuko juu ya ´Arshi. Lakini Jahmiyyah wanasema: "Hakuna mungu yeyote juu ya ´Arshi.'" 2) 'Abbaad bin al-' Awaam (d. 185) kasema: "Niliongea na Bishr al-Mariysiy na wafuasi wake na mwishowe nikaja kujua ya kwamba wanasema hakuna mungu yeyote juu ya mbingu. Naonelea ya kwamba mtu asichanganyike nao katika kuoana wala mtu asiwarithi.” 3) al-Asma'iyl (d. 213) kasema: "Mke wa Jahm alikuja wakati mtu alimwambia kuwa Allaah Yuko juu ya ´Arshi. Alisema: "Ni Mwenye mpaka juu ya kitu chenye mpaka?" Mwanamke huyu ni kafiri (Kaafirah) kwa sababu ya kauli hii." 4) Muhammad bin Mus'ab (d. 228) kasema: "Yule anayedai ya kwamba Husemi na kwamba hutoonekana siku ya Qiyaamah basi hakuamini. Nashuhudia ya kwamba Uko juu ya ´Arshi, juu ya mbingu hizi saba, na si kama wazushi wanavyosema." 5) Wahb bin Jariyr (d. 206) kasema: "Kaa mbali na maoni ya Jahm! Wao wamejadiliana na mimi kwamba hakuna mungu juu ya mbingu. Huo ufunuo kutoka kwa Ibliys. Hilo si kitu jengine zaidi na kutokuamini (Kufr). " 6) Swaalih bin Adh-Dhuray kasema: "Kuna mtu mmoja alifungwa kwa kuwa alikuwa na ´Aqiydah ya Jahmiyyah. Baada ya muda, akatubu. Wakampeleka kwa Hishaam bin ´Ubaydillaah ili kumjaribu. Akasema: “Je, unaamani ya kwamba Allaah Yuko juu ya ´Arshi Yake?” Akasema: “Sijui ni nani ambaye ametoka katika uumbaji wake.” Hivyo akasema Hishaam "Mrudisheni gerezaki. Hakutubia." Hishaam bin 'Ubaydillaah alikuwa ni mmoja katika wanachioni anaefuata madhehebu ya Abu Haniyfah. 7) Abu Ma'mar Qatiy'iy (d. 236) kasema: "Maoni ya Jahmiyyah yanaishia kwa kusema kwamba hakuna mungu yeyote juu ya mbingu." 8) Bishr al-Haafiy (d. 227) kasema: "Tunamuamini ya kwamba Allaah Kastawaa juu ya ´Arshi Yake vile Apendavyo na kwamba Anajua kila kitu." 9) Yuusuf bin Muusa kasema: "Kulisemwa kuambiwa Abu ´Abdillaah Ahmad bin Hanbal "Je, Allaah Yuko juu ya mbingu hizi saba, juu ya ´Arshi na katoka katika uumbaji Wake wakati nguvu na elimu Yake viko kila mahali?" Akasema: "Ndiyo." 10) 'Abdul-Wahhaab bin ´Abdil-Hakam (d. 251), mwalimu wa Abu Daawuud, kasema: "Yule ambaye anasema kuwa Allaah Yuko hapa ni Jahmiy. Hakika Allaah Yuko juu ya ´Arshi Yake na elimu Yake imekizunguka kila kitu katika maisha haya na maisha baada ya haya." Mwandishi: Imaam Shams-ud-Diyn bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (d. 744) Chanzo: Al-Istiwaa' 'alaal-'Arsh, uk. 57-66

1) Sa´iyd bin ´Aamir adh-Dhab’iy (d. 208) – Imaam wa Basrah – kasema:
“Jahmiyyah wana mtazamo mbaya zaidi kuliko Mayahudi na Wakristo. Dini zote ikiwa ni pamoja na Waislamu wamekubaliana ya kwamba Allaah Yuko juu ya ´Arshi. Lakini Jahmiyyah wanasema: “Hakuna mungu yeyote juu ya ´Arshi.'”

2) ‘Abbaad bin al-‘ Awaam (d. 185) kasema:
“Niliongea na Bishr al-Mariysiy na wafuasi wake na mwishowe nikaja kujua ya kwamba wanasema hakuna mungu yeyote juu ya mbingu. Naonelea ya kwamba mtu asichanganyike nao katika kuoana wala mtu asiwarithi.”

3) al-Asma’iyl (d. 213) kasema:
“Mke wa Jahm alikuja wakati mtu alimwambia kuwa Allaah Yuko juu ya ´Arshi. Alisema: “Ni Mwenye mpaka juu ya kitu chenye mpaka?” Mwanamke huyu ni kafiri (Kaafirah) kwa sababu ya kauli hii.”

4) Muhammad bin Mus’ab (d. 228) kasema:
“Yule anayedai ya kwamba Husemi na kwamba hutoonekana siku ya Qiyaamah basi hakuamini. Nashuhudia ya kwamba Uko juu ya ´Arshi, juu ya mbingu hizi saba, na si kama wazushi wanavyosema.”

5) Wahb bin Jariyr (d. 206) kasema:
“Kaa mbali na maoni ya Jahm! Wao wamejadiliana na mimi kwamba hakuna mungu juu ya mbingu. Huo ufunuo kutoka kwa Ibliys. Hilo si kitu jengine zaidi na kutokuamini (Kufr). ”

6) Swaalih bin Adh-Dhuray kasema:
“Kuna mtu mmoja alifungwa kwa kuwa alikuwa na ´Aqiydah ya Jahmiyyah. Baada ya muda, akatubu. Wakampeleka kwa Hishaam bin ´Ubaydillaah ili kumjaribu. Akasema: “Je, unaamani ya kwamba Allaah Yuko juu ya ´Arshi Yake?” Akasema: “Sijui ni nani ambaye ametoka katika uumbaji wake.” Hivyo akasema Hishaam “Mrudisheni gerezaki. Hakutubia.”
Hishaam bin ‘Ubaydillaah alikuwa ni mmoja katika wanachioni anaefuata madhehebu ya Abu Haniyfah.

7) Abu Ma’mar Qatiy’iy (d. 236) kasema:
“Maoni ya Jahmiyyah yanaishia kwa kusema kwamba hakuna mungu yeyote juu ya mbingu.”

8) Bishr al-Haafiy (d. 227) kasema:
“Tunamuamini ya kwamba Allaah Kastawaa juu ya ´Arshi Yake vile Apendavyo na kwamba Anajua kila kitu.”

9) Yuusuf bin Muusa kasema:
“Kulisemwa kuambiwa Abu ´Abdillaah Ahmad bin Hanbal “Je, Allaah Yuko juu ya mbingu hizi saba, juu ya ´Arshi na katoka katika uumbaji Wake wakati nguvu na elimu Yake viko kila mahali?” Akasema: “Ndiyo.”

10) ‘Abdul-Wahhaab bin ´Abdil-Hakam (d. 251), mwalimu wa Abu Daawuud, kasema:
“Yule ambaye anasema kuwa Allaah Yuko hapa ni Jahmiy. Hakika Allaah Yuko juu ya ´Arshi Yake na elimu Yake imekizunguka kila kitu katika maisha haya na maisha baada ya haya.”

Mwandishi: Imaam Shams-ud-Diyn bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (d. 744)
Chanzo: Al-Istiwaa’ ‘alaal-‘Arsh, uk. 57-66


  • Kitengo: Uncategorized , Kuwa juu kwa Allaah
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013