Hadiyth Dhaifu Ya Mu´aadh (Radhiya Allaahu ´anhu)

Shaykh Abu´Abdul-Haliym ´Abdul-Haadiy: Kwa kuwa kuna baadhi ya Hadiyth ambazo Ummah wamezikubali, ila hazikuthibiti kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama Hadityh mash-huri wakati Mtume alipomtume Mu´aadh (Radhiya Allaahu ´anhu) kwenda Yemen. “Akamwambia utahukumu kwa kitu gani? (Mu´aadh) akasema: “Kwa Kitabu cha Allaah (Qur-aan)." (Mtume) Akamuuliza "Ikiwa hukupata katika Kitabu cha Allaah?” Akasema "Kwa Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla allaahu ´alayhi wa sallam)." Akamuuliza “Ikiwa hukupata katika Sunnah za Mtume wa Allaah?” Akasema "Ntajitahidi kwa rai yangu." Hadiyth hii enyi waja wa Allaah, haikuthibiti kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hata kama Ummah wameikubali. Ni wajibu kutanabahi jambo hili.

Shaykh Abu´Abdul-Haliym ´Abdul-Haadiy:

Kwa kuwa kuna baadhi ya Hadiyth ambazo Ummah wamezikubali, ila hazikuthibiti kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama Hadityh mash-huri wakati Mtume alipomtume Mu´aadh (Radhiya Allaahu ´anhu) kwenda Yemen.

“Akamwambia utahukumu kwa kitu gani? (Mu´aadh) akasema: “Kwa Kitabu cha Allaah (Qur-aan).” (Mtume) Akamuuliza “Ikiwa hukupata katika Kitabu cha Allaah?” Akasema “Kwa Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla allaahu ´alayhi wa sallam).” Akamuuliza “Ikiwa hukupata katika Sunnah za Mtume wa Allaah?” Akasema “Ntajitahidi kwa rai yangu.”

Hadiyth hii enyi waja wa Allaah, haikuthibiti kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hata kama Ummah wameikubali. Ni wajibu kutanabahi jambo hili.