´Amali Za Muislamu Mwenye Kuritadi

Swali La Kwanza: Mwenye kusema neno akaritadi kwalo kutoka katika Dini yake ´amali zake zote zinaporomoka (haribika)? ´Allaamah al-Fawzaan: Kuritadi kunaharibu ´amali zote mpaka mtu atubu kwa Allaah (´Azza wa Jalla). Na mwenye kutubia, Allaah Humsamehe. Swali La Pili: Na ´amali zake zikishaharibika na akarejea katika Uislamu. Je, anarudishiwa ´amali zake (nzuri) zilizotangulia? ´Allaamah al-Fawzaan: Hapa ndipo mahali ya tofauti. Katika wanachuoni kuko ambao wanasema harudishiwi. Ataanza upya. Na katika wao kuko wanaosema anarudishiwa, na katika wao ni Imaam ash-Shaafi´iy. Na hilo ni kutokana na Kauli Yake (Ta´ala): وَمَن يَرْتَدِدْ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَيَمُتْ وَهُوَ كَافِرٌ فَأُولَـٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ "Na atakayeritadi miongoni mwenu kutoka Dini yake, akafariki hali ya kuwa ni kafiri, basi hao zimeharibika ‘amali zao katika dunia na Aakhirah." (02:217) Kafanya kuharibika kwa ´amali ni kwa mambo mawili: 1) Kuritadi na 2) kwa mauti juu yayo. Ni dalili ya kwamba lau atatubu kabla ya kufa ´amali zake zinamrudilia. Na (kauli) hii ndio nilikuwa namsikia Shaykh Ibn Baaz akiona kuwa ndio yenye nguvu.

Swali La Kwanza:
Mwenye kusema neno akaritadi kwalo kutoka katika Dini yake ´amali zake zote zinaporomoka (haribika)?

´Allaamah al-Fawzaan:
Kuritadi kunaharibu ´amali zote mpaka mtu atubu kwa Allaah (´Azza wa Jalla). Na mwenye kutubia, Allaah Humsamehe.

Swali La Pili:
Na ´amali zake zikishaharibika na akarejea katika Uislamu. Je, anarudishiwa ´amali zake (nzuri) zilizotangulia?

´Allaamah al-Fawzaan:
Hapa ndipo mahali ya tofauti. Katika wanachuoni kuko ambao wanasema harudishiwi. Ataanza upya. Na katika wao kuko wanaosema anarudishiwa, na katika wao ni Imaam ash-Shaafi´iy. Na hilo ni kutokana na Kauli Yake (Ta´ala):

وَمَن يَرْتَدِدْ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَيَمُتْ وَهُوَ كَافِرٌ فَأُولَـٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ
“Na atakayeritadi miongoni mwenu kutoka Dini yake, akafariki hali ya kuwa ni kafiri, basi hao zimeharibika ‘amali zao katika dunia na Aakhirah.” (02:217)

Kafanya kuharibika kwa ´amali ni kwa mambo mawili: 1) Kuritadi na 2) kwa mauti juu yayo. Ni dalili ya kwamba lau atatubu kabla ya kufa ´amali zake zinamrudilia. Na (kauli) hii ndio nilikuwa namsikia Shaykh Ibn Baaz akiona kuwa ndio yenye nguvu.