´Allaamah al-Fawzaan Kuhusu Mtazamo Wa al-Qaradhwaawiy Kwa Paulo

Yusuuf al-Qaradhwaawiy anasema: "Leo sisi tutaongelea kuhusu utu. Hata hivyo, si utu wa Kiislamu, bali ni wa Kikristo. Ni kuhusiana na Papa Yohane Paulo II, Vatican na Kanisa la Katoliki. Ni mtu mkubwa katika Ukristo. Kafariki jana, jambo ambalo limeeenea duniani kote. Ni wajibu wetu kuwapa pole ulimwengu wa Kikristo na mapadiri wa Wakristo katika Vatican na duniani kote. Baadhi yao ni marafiki zetu ambao tumekutana nao mara kwa mara katika mikutano, semina na majadiliano. Tunawatumia pole kutokana na kifo cha padiri huyu mkubwa ambaye Wakristo huwa wanamchagua mwenyewe kwa khiyari. Sisi Waislamu tuna ndoto kwa jamii ya wanachuoni kuweza kuchagua Shaykh mkuu, au Imaam mkuu, na si kwamba atateuliwa na nchi au Serikali. Tunatoa pole zetu kwa Papa ambaye alikuwa na nafasi inayofaa kupongezwa, ingawa baadhi ya Waislamu wanasema kuwa hakuomba radhi kwa mambo ambayo Waislamu wamekabiliwa wakati wa misalaba kama ambavyo aliwaomba radhi Mayahudi na mambo mengine ambayo walimkosoa kwayo. Hata hivyo, sisi tunaongelea nafasi ya mtu huyu kwa jumla, juhudi zake na Ikhlaasw aliyokuwa nayo ya usambazaji wa Dini yake. Licha ya umri wake mkubwa aliyokuwa nao, anasafiri kote duniani na wakati mwingine katika nchi za Kiislamu. Alikuwa mkweli katika Dini yake na juhudi tukija kwa kuieneza na kuamini ujumbe wake. Alikuwa na nafasi ya kisiasa ambayo itaandikwa katika matendo yake mema. Alikuwa ni mtu wa amani mwenye kuita katika amani. Alikuwa dhidi ya vita nchini Iraq. Alikuwa dhidi ya kizuizi Palestina . Ana nafasi kuu kama tulivyosema. Tunamuomba Allaah Amrehemu na Amlipe kwa wema aliyoufanya wa kibinaadamu na uzuri aliyouacha. Tunatuma pole zetu kwa Wakristo wote duniani na marafiki zetu Roma. Tunamuomba Allaah Awape ulimwengu wa Kikristo mrithi bora." Swali: Kuna mtu mmoja katika wale wanaotoa Fatwa kwenye chaneli ya Al Jazeera anasema ni wajibu wa Waislamu kuwapa pole Wakristo, na kwamba moja ya fadhila za Papa ilikuwa ni yeye kueneza Dini yake kwa Ikhlaasw na kasema ya kwamba amemuomba Allaah Amrehemu na Amsamehe, na kwamba Wakristo wapate mrithi bora. Nini hukumu ya hili? ´Allaamah al-Fawzaan: Hili hali kadhalika ni kama lile kikundi lingine tulilosema. Hawataki kuwa na mapenzi na chuki kwa ajili ya Allaah. Wanataka watu wote wawe sawa. Wakristo, Waislamu na Mayahudi. Ukweli ni kwamba hawataki hata wawe sawa sawa. Wanachotaka ni Uyahudi na Ukristo. Wanasema hivi kwa ajili tu ya adabu. Vinginevyo, hakuna kitu wanachokichukia sana kama Uislamu. Wanapenda Uyahudi na Ukristo, lakini hapana Uislamu. Maneno ya mtu huyu yapuuzwe, bila kujaliwa sawa kama yamesemwa kwenye vyombo vya habari au mahali pengine. Ni wajibu kukataa maneno yake na kukaa mbali na wao.

Yusuuf al-Qaradhwaawiy anasema:

“Leo sisi tutaongelea kuhusu utu. Hata hivyo, si utu wa Kiislamu, bali ni wa Kikristo. Ni kuhusiana na Papa Yohane Paulo II, Vatican na Kanisa la Katoliki. Ni mtu mkubwa katika Ukristo. Kafariki jana, jambo ambalo limeeenea duniani kote.

Ni wajibu wetu kuwapa pole ulimwengu wa Kikristo na mapadiri wa Wakristo katika Vatican na duniani kote. Baadhi yao ni marafiki zetu ambao tumekutana nao mara kwa mara katika mikutano, semina na majadiliano. Tunawatumia pole kutokana na kifo cha padiri huyu mkubwa ambaye Wakristo huwa wanamchagua mwenyewe kwa khiyari.

Sisi Waislamu tuna ndoto kwa jamii ya wanachuoni kuweza kuchagua Shaykh mkuu, au Imaam mkuu, na si kwamba atateuliwa na nchi au Serikali.

Tunatoa pole zetu kwa Papa ambaye alikuwa na nafasi inayofaa kupongezwa, ingawa baadhi ya Waislamu wanasema kuwa hakuomba radhi kwa mambo ambayo Waislamu wamekabiliwa wakati wa misalaba kama ambavyo aliwaomba radhi Mayahudi na mambo mengine ambayo walimkosoa kwayo.

Hata hivyo, sisi tunaongelea nafasi ya mtu huyu kwa jumla, juhudi zake na Ikhlaasw aliyokuwa nayo ya usambazaji wa Dini yake. Licha ya umri wake mkubwa aliyokuwa nao, anasafiri kote duniani na wakati mwingine katika nchi za Kiislamu. Alikuwa mkweli katika Dini yake na juhudi tukija kwa kuieneza na kuamini ujumbe wake. Alikuwa na nafasi ya kisiasa ambayo itaandikwa katika matendo yake mema.

Alikuwa ni mtu wa amani mwenye kuita katika amani. Alikuwa dhidi ya vita nchini Iraq. Alikuwa dhidi ya kizuizi Palestina . Ana nafasi kuu kama tulivyosema. Tunamuomba Allaah Amrehemu na Amlipe kwa wema aliyoufanya wa kibinaadamu na uzuri aliyouacha. Tunatuma pole zetu kwa Wakristo wote duniani na marafiki zetu Roma. Tunamuomba Allaah Awape ulimwengu wa Kikristo mrithi bora.”

Swali:
Kuna mtu mmoja katika wale wanaotoa Fatwa kwenye chaneli ya Al Jazeera anasema ni wajibu wa Waislamu kuwapa pole Wakristo, na kwamba moja ya fadhila za Papa ilikuwa ni yeye kueneza Dini yake kwa Ikhlaasw na kasema ya kwamba amemuomba Allaah Amrehemu na Amsamehe, na kwamba Wakristo wapate mrithi bora. Nini hukumu ya hili?

´Allaamah al-Fawzaan:
Hili hali kadhalika ni kama lile kikundi lingine tulilosema. Hawataki kuwa na mapenzi na chuki kwa ajili ya Allaah. Wanataka watu wote wawe sawa. Wakristo, Waislamu na Mayahudi. Ukweli ni kwamba hawataki hata wawe sawa sawa. Wanachotaka ni Uyahudi na Ukristo. Wanasema hivi kwa ajili tu ya adabu. Vinginevyo, hakuna kitu wanachokichukia sana kama Uislamu. Wanapenda Uyahudi na Ukristo, lakini hapana Uislamu. Maneno ya mtu huyu yapuuzwe, bila kujaliwa sawa kama yamesemwa kwenye vyombo vya habari au mahali pengine. Ni wajibu kukataa maneno yake na kukaa mbali na wao.