al-Faakihaaniy Kuhusu Sherehe Ya Maulidi

Watu wema wameuliza mara nyingi swali kuhusu ukusanyikaji unaofanyika na baadhi ya watu katika Rabiy´ al-Awwal, ambao wanaiita "Maulidi". Je, yana msingi katika Dini? Wanataka jibu la ufafanuuzi. Nikajibu na kwa Allaah ndio kwenye mafanikio: Sijui kuwa Maulidi haya yana msingi katika Qur-aan au Sunnah. Na haijathibiti kutoka kwa mwanachuoni yeyote wa Ummah ambaye ni ruwaza njema katika Dini na ambaye anashikamana na wakale. Ukweli ni kwamba jambo hili ni Bid´ah. Yalizushwa na wavivu na watu waroho. Dalili ya hilo ni kwamba, ikiwa tutayakutanisha na zile hukumu tano, tungelisema kuwa jambo hili ima ni wajibu, limependekezwa, linaruhusiwa, linachukiza au haramu pia. Ni jambo waislamu wamekubaliana ya kwamba si wajibu au kupendekezwa. Jambo lililopendekezwa ni jambo ambalo Shari´ah imeliamrisha bila ya kumhukumu (dhambi) yule ambaye hakulifanya. Jambo hili Shari'ah haikuliruhusu. Maswahabah na waliokuja baada yao hawakulifanya. Na wala sijui ya kwamba wanachuoni wa Dini walilifanya. Hili ndio jibu langu mbele ya Allaah (Ta´ala) ikiwa nitaulizwa kuhusu hilo. Hayawezi pia kuwa yanaruhusiwa kwa sababu jamhuri imekubaliana ya kwamba ni haramu kuzusha katika Dini. Hivyo, jambo hili linaweza kuwa ima lenye kuchukiza au haramu pia. Katika hali hii mtu anaweza kuyaongelea katika njia mbili tofauti: Jambo la kwanza: Mtu kufanya hilo na mke wake, rafiki zake na familia yake, kuyasimamia kwa pesa zake mwenyewe na kula tu wakati wa mkusanyiko bila ya kushiriki dhambi yoyote. Ni mkusanyiko huu ndio tunauelezea kuwa ni Bid´ah yenye kuchukiza na kitendo cha machukizo. Kwa maana hakuna mtu yeyote katika karne za kale, ambaye ni mwanachuoni wa Uislamu na watu aliyeyafanya. Jambo la pili: Kwamba dhambi imeshiriki [katika Maulidi hayo] na mtu anaomba wengine pesa kwa ajili yake. Roho imejisalimisha kwa hilo wakati moyo unateseka kwa mateso ya dhuluma. Baadhi ya wanachuoni wamesema: "Kuchukua pesa kwa kustahi ni kama kuzichukua kwa upanga." Na hili ni hususan pale ambapo mkusanyiko unafuatana na nyimbo na vyombo kama matari na vijana wanawake na wanaume ambao wanakaa pamoja na vijana wasiokuwa na ndevu na waimbaji. Hili linaweza kufanyika kwa mchanganyiko wa moja kwa moja au kwamba wanawake kuwahudumia wanaume na kucheza kwa kuamsha hisia. Aidha, mkusanyiko unakuwa na burudani zisizohitajika ambapo husahau Siku ya Qiyaamah. Hali kadhalika wanawake wanapokusanyika wao wenyewe, kupandisha sauti zao, kuimba na kushindwa kusoma na kumkumbuka Allaah kwa njia ya kidini na ya kawaida. Wanapuuza Maneno ya Allaah (Ta´ala): إن ربك لبالمرصاد “Hakika Mola wako bila shaka Yuko katika Kuchunga (na kuwavizia).” (89:14) Hakuna yeyote anayeonelea hili linajuzu. Si mwenye heshima, busara na wanaume shujaa kuona hili ni zuri. Watu ambao wanaruhusu jambo hili ni wale wenye mioyo ya maradhi ambao hawaachi dhambi. Na hawakutosheka na hilo, wanafikia mpaka kusema hata ya kwamba jambo hili ni aina ya ´Ibaadah na halikukatazwa. Inna liLlaahi wa inna Ilayhi raaji´uun. Uislamu ulianza kitu kigeni na utarudi kuwa kama ulivyoanza. Imaam Abu 'Amr bin al-' Alaa' kapatia aliposema: "Watu watakuwa katika hali nzuri maadamu wanastaajabu katika ajabu." Isitoshe mwezi huu - Rabiy' al-Awwal – ambao Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alizaliwa katika mwezi huo, ni mwezi huo huo alifariki. Hakuna haki zaidi ya kufurahia katika mwezi huo kuliko kusikitika. Hili ndio nimelazimika kwangu kulisema. Ninamuomba Allaah Ataqabali ´amali hii. Mwandishi: Imaam Abu Hafs Taaj-ud-Diyn al-Faakihaaniy (d. 734) al-Mawrid fiy 'Amal-il-Mawlid, uk. 20-27

Watu wema wameuliza mara nyingi swali kuhusu ukusanyikaji unaofanyika na baadhi ya watu katika Rabiy´ al-Awwal, ambao wanaiita “Maulidi”. Je, yana msingi katika Dini? Wanataka jibu la ufafanuuzi. Nikajibu na kwa Allaah ndio kwenye mafanikio:

Sijui kuwa Maulidi haya yana msingi katika Qur-aan au Sunnah. Na haijathibiti kutoka kwa mwanachuoni yeyote wa Ummah ambaye ni ruwaza njema katika Dini na ambaye anashikamana na wakale. Ukweli ni kwamba jambo hili ni Bid´ah. Yalizushwa na wavivu na watu waroho. Dalili ya hilo ni kwamba, ikiwa tutayakutanisha na zile hukumu tano, tungelisema kuwa jambo hili ima ni wajibu, limependekezwa, linaruhusiwa, linachukiza au haramu pia.

Ni jambo waislamu wamekubaliana ya kwamba si wajibu au kupendekezwa. Jambo lililopendekezwa ni jambo ambalo Shari´ah imeliamrisha bila ya kumhukumu (dhambi) yule ambaye hakulifanya. Jambo hili Shari’ah haikuliruhusu. Maswahabah na waliokuja baada yao hawakulifanya. Na wala sijui ya kwamba wanachuoni wa Dini walilifanya. Hili ndio jibu langu mbele ya Allaah (Ta´ala) ikiwa nitaulizwa kuhusu hilo.
Hayawezi pia kuwa yanaruhusiwa kwa sababu jamhuri imekubaliana ya kwamba ni haramu kuzusha katika Dini.
Hivyo, jambo hili linaweza kuwa ima lenye kuchukiza au haramu pia. Katika hali hii mtu anaweza kuyaongelea katika njia mbili tofauti:

Jambo la kwanza: Mtu kufanya hilo na mke wake, rafiki zake na familia yake, kuyasimamia kwa pesa zake mwenyewe na kula tu wakati wa mkusanyiko bila ya kushiriki dhambi yoyote. Ni mkusanyiko huu ndio tunauelezea kuwa ni Bid´ah yenye kuchukiza na kitendo cha machukizo. Kwa maana hakuna mtu yeyote katika karne za kale, ambaye ni mwanachuoni wa Uislamu na watu aliyeyafanya.

Jambo la pili: Kwamba dhambi imeshiriki [katika Maulidi hayo] na mtu anaomba wengine pesa kwa ajili yake. Roho imejisalimisha kwa hilo wakati moyo unateseka kwa mateso ya dhuluma. Baadhi ya wanachuoni wamesema:

“Kuchukua pesa kwa kustahi ni kama kuzichukua kwa upanga.”

Na hili ni hususan pale ambapo mkusanyiko unafuatana na nyimbo na vyombo kama matari na vijana wanawake na wanaume ambao wanakaa pamoja na vijana wasiokuwa na ndevu na waimbaji. Hili linaweza kufanyika kwa mchanganyiko wa moja kwa moja au kwamba wanawake kuwahudumia wanaume na kucheza kwa kuamsha hisia. Aidha, mkusanyiko unakuwa na burudani zisizohitajika ambapo husahau Siku ya Qiyaamah.
Hali kadhalika wanawake wanapokusanyika wao wenyewe, kupandisha sauti zao, kuimba na kushindwa kusoma na kumkumbuka Allaah kwa njia ya kidini na ya kawaida. Wanapuuza Maneno ya Allaah (Ta´ala):

إن ربك لبالمرصاد
“Hakika Mola wako bila shaka Yuko katika Kuchunga (na kuwavizia).” (89:14)

Hakuna yeyote anayeonelea hili linajuzu. Si mwenye heshima, busara na wanaume shujaa kuona hili ni zuri. Watu ambao wanaruhusu jambo hili ni wale wenye mioyo ya maradhi ambao hawaachi dhambi. Na hawakutosheka na hilo, wanafikia mpaka kusema hata ya kwamba jambo hili ni aina ya ´Ibaadah na halikukatazwa. Inna liLlaahi wa inna Ilayhi raaji´uun. Uislamu ulianza kitu kigeni na utarudi kuwa kama ulivyoanza.
Imaam Abu ‘Amr bin al-‘ Alaa’ kapatia aliposema:

“Watu watakuwa katika hali nzuri maadamu wanastaajabu katika ajabu.”

Isitoshe mwezi huu – Rabiy’ al-Awwal – ambao Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alizaliwa katika mwezi huo, ni mwezi huo huo alifariki. Hakuna haki zaidi ya kufurahia katika mwezi huo kuliko kusikitika.
Hili ndio nimelazimika kwangu kulisema. Ninamuomba Allaah Ataqabali ´amali hii.

Mwandishi: Imaam Abu Hafs Taaj-ud-Diyn al-Faakihaaniy (d. 734)
al-Mawrid fiy ‘Amal-il-Mawlid, uk. 20-27


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 24th, October 2013