al-Ajurriy Kuhusu Kuwa Juu Kwa Allaah

Kwa upande mwingine, wanasema wanachuoni ya kwamba Allaah ('Azza wa Jalla) Yuko juu ya ´Arshi Yake juu ya mbingu Zake. Elimu Yake imekienea (imekizunguka) kila kitu. Ana ujuzi wa kila kitu Alichokiumba mbinguni, katika ardhi na kati ya hivyo viwili. Ana ujuzi wa vya siri na vilivyojificha. Ana ujuzi wa matakwa na mawazo. Anasikia na Anaona. Hivyo, Yeye (Subhaanahu) Yuko juu ya ´Arshi Yake. Kwake hupanda matendo mema ya waja. Yanayotoa ushahidi wa hilo katika Kitabu Chake, miongoni mwa dalili hizo ni Kauli Yake: أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاء أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُور ”Mnadhani mko salama kwa alioko juu kuwa hatakudidimizeni kwenye ardhi, na tahamaki hiyo inatikisika!” (67 : 16) إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ “Kwake hupanda neno zuri (dhikru-Allaah), na kitendo chema (cha ikhlaasw) Hukipa hadhi (Hukitakabali).” (35 : 10) يَا عِيسَىٰ إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ “Ee ‘Iysaa, hakika Mimi ni Mwenye kukuchukua na Mwenye kukupandisha Kwangu.” (03 : 55) بَل رَّفَعَهُ اللَّـهُ إِلَيْهِ ”Bali Allaah Alimnyanyua Kwake.” (04 : 158) Mwandishi: Abu Bakr Muhammad bin al-Husayn al-Ajurriy (d. 360) Chanzo: ash-Shari'ah, uk. 292

Kwa upande mwingine, wanasema wanachuoni ya kwamba Allaah (‘Azza wa Jalla) Yuko juu ya ´Arshi Yake juu ya mbingu Zake. Elimu Yake imekienea (imekizunguka) kila kitu. Ana ujuzi wa kila kitu Alichokiumba mbinguni, katika ardhi na kati ya hivyo viwili. Ana ujuzi wa vya siri na vilivyojificha. Ana ujuzi wa matakwa na mawazo. Anasikia na Anaona. Hivyo, Yeye (Subhaanahu) Yuko juu ya ´Arshi Yake. Kwake hupanda matendo mema ya waja.

Yanayotoa ushahidi wa hilo katika Kitabu Chake, miongoni mwa dalili hizo ni Kauli Yake:

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاء أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُور
”Mnadhani mko salama kwa alioko juu kuwa hatakudidimizeni kwenye ardhi, na tahamaki hiyo inatikisika!” (67 : 16)

إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ
“Kwake hupanda neno zuri (dhikru-Allaah), na kitendo chema (cha ikhlaasw) Hukipa hadhi (Hukitakabali).” (35 : 10)

يَا عِيسَىٰ إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ
“Ee ‘Iysaa, hakika Mimi ni Mwenye kukuchukua na Mwenye kukupandisha Kwangu.” (03 : 55)

بَل رَّفَعَهُ اللَّـهُ إِلَيْهِ
”Bali Allaah Alimnyanyua Kwake.” (04 : 158)

Mwandishi: Abu Bakr Muhammad bin al-Husayn al-Ajurriy (d. 360)
Chanzo: ash-Shari’ah, uk. 292


  • Kitengo: Uncategorized , Kuwa juu kwa Allaah
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013