Ahl-us-Sunnah Wanawapenda Maimamu Na Wanachuoni Wote

´Allaamah al-Waadi´iy: Sisi tuko na Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Isitoshe Ahl-us-Sunnah wanawapenda Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mapenzi ya Kidini. Na wanawapenda maimamu wa Hadiyth mapenzi ya Kidini. Na wanawapenda maimamu watukufu kama Imaam Ahmad, Imaam Maalik na Imaam ash-Shaafi´iy (Rahimahumu Allaah) mapenzi ya Kidini. Tofauti na wale wanaofuata madhehebu kichwa mchunga. Ukisoma vitabu vya historia, kama "al-Bidaayah wan-Nihaayah" cha Ibn Kathiyr utaona kulivyokuwa ugomvi na fitina Misikitini. Bali baya zaidi kuliko hili, katika al-Masjid al-Haraam kulikuwa kunaswali madhehebu manne kila mmoja na Swalah yake. Kila dhehebu lilikuwa na imamu wake na wanaswali nyuma yake. Waislamu walikuwa haswali Swalah moja kwa pamoja mpaka likandolewa katika muda ambao si mbali sana. Sisi Ahl-us-Sunnah - Alhamduli Allaah - tunawapenda wanachuoni wote. Na wala hatumfuati kichwa mchunga yeyote katika wao.

´Allaamah al-Waadi´iy:

Sisi tuko na Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Isitoshe Ahl-us-Sunnah wanawapenda Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mapenzi ya Kidini. Na wanawapenda maimamu wa Hadiyth mapenzi ya Kidini. Na wanawapenda maimamu watukufu kama Imaam Ahmad, Imaam Maalik na Imaam ash-Shaafi´iy (Rahimahumu Allaah) mapenzi ya Kidini. Tofauti na wale wanaofuata madhehebu kichwa mchunga. Ukisoma vitabu vya historia, kama “al-Bidaayah wan-Nihaayah” cha Ibn Kathiyr utaona kulivyokuwa ugomvi na fitina Misikitini. Bali baya zaidi kuliko hili, katika al-Masjid al-Haraam kulikuwa kunaswali madhehebu manne kila mmoja na Swalah yake. Kila dhehebu lilikuwa na imamu wake na wanaswali nyuma yake. Waislamu walikuwa haswali Swalah moja kwa pamoja mpaka likandolewa katika muda ambao si mbali sana. Sisi Ahl-us-Sunnah – Alhamduli Allaah – tunawapenda wanachuoni wote. Na wala hatumfuati kichwa mchunga yeyote katika wao.