30. Aina za shirki na baadhi ya mifano

Mosi: Shirki kubwa: Nako ni kama kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah, kumuomba asiyekuwa Allaah, kusujudu kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, kama kuamini asiyekuwa Allaah anaweza kunufaisha au kudhuru badala ya Allaah. Mwenye kufanya hivyo anatoka katika dini. Pili: Shirki ndogo: Ni kama Riyaa ndogo. Mwenye Riyaa hii hatoki katika Dini, lakini inawajibisha kutubia kwayo. Tatu: Shirki iliyofichikana: Nayo ni mtu kufanya ´amali nafasi ya mtu, nayo ni shirki ndogo lakini ni dhambi kubwa. Miongoni mwayo ni Riyaa. Shirki hii haimtoi mtu katika Uislamu lakini inawajibisha kutubia. Kuhusu shirki kubwa inamtoa mtu katika Uislamu. Nne: Shirki ya I´tiqaad: Ni mtu kuamini ya kwamba asiyekuwa Allaah anaumba, anaruzuku, anahuisha, anafisha au anajua yaliyofichikana isipokuwa Allaah. Hii ni shirki kubwa nayo inamtoa katika Uislamu. Tano: Shirki ya kimatendo: Ni kila tendo lililohukumiwa na Shari´ah ya kwamba ni shirki. Shirki hii kuna kubwa na ndogo. Sita: Shirki ya kimatamshi: Ni kila tamshi lililohukumiwa na Shari´ah ya kwamba ni shirki. Kwa mfano kuapa kwa asiyekuwa Allaah, kama wasemavyo baadhi ya watu: ´Sikuwa mimi isipokuwa kwa ajili ya Allaah na kwa ajili yako`, ´namtegemea Allaah na wewe`, ´lau bila ya Allaah na fulani kusingelikuwa kadhaa`, na matamshi mengineyo ya shirki. Shirki hii kuna kubwa na ndogo. Saba: Shirki ya kutunga Shari´ah: Ni mtu kuipuuza Qur-aan na Sunnah au akapuuza baadhi ya hukumu zake. Badala yake akachukua maoni na kanuni za watu. Allaah (Ta´ala) amesema: أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ “Je, wanao washirika waliowaamuru dini yale ambayo Allaah Hakuyatolea kwayo idhini?” (42:21) Nane: Shirki ya mapenzi: Ni kule mtu kumpenda asiyekuwa Allaah kama jinsi anavyompenda Allaah au zaidi. Anasema Allaah (Ta´ala): وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ “Na miongoni mwa watu wako wenye kuchukua asiyekuwa Allaah kuwa ni wanaolingana [na Allaah] wanawapenda kama mapenzi ya kumpenda Allaah.” (02:165) Tisa: Shirki ya khofu na kuogopa: Tutalizungumzia katika “Vigawanyo vya khofu” - Allaah akitaka. Kumi: Shirki ya makusudio na matakwa: Ni mtu afanye ´amali na huku asimkusudii na wala asifanye kwa ajili ya Allaah. Hii ni shirki ya makusudio na matakwa. Kumi na moja: Shirki ya utiifu: Ni kule mja kumtii mtu katika kuhalalisha haramu au kuharamisha halali. Amesema (Ta´ala): اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ “Wamewafanya marabi na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Allaah.” (09:31) Mwandishi: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy Chanzo: al-Qawl al-Mufiyd fiy Adillat-it-Tawhiyd Toleo la: 15.08.2015 Tarjama: Wanachuoni.com

Mosi: Shirki kubwa: Nako ni kama kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah, kumuomba asiyekuwa Allaah, kusujudu kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, kama kuamini asiyekuwa Allaah anaweza kunufaisha au kudhuru badala ya Allaah. Mwenye kufanya hivyo anatoka katika dini.

Pili: Shirki ndogo: Ni kama Riyaa ndogo. Mwenye Riyaa hii hatoki katika Dini, lakini inawajibisha kutubia kwayo.

Tatu: Shirki iliyofichikana: Nayo ni mtu kufanya ´amali nafasi ya mtu, nayo ni shirki ndogo lakini ni dhambi kubwa. Miongoni mwayo ni Riyaa. Shirki hii haimtoi mtu katika Uislamu lakini inawajibisha kutubia. Kuhusu shirki kubwa inamtoa mtu katika Uislamu.

Nne: Shirki ya I´tiqaad: Ni mtu kuamini ya kwamba asiyekuwa Allaah anaumba, anaruzuku, anahuisha, anafisha au anajua yaliyofichikana isipokuwa Allaah. Hii ni shirki kubwa nayo inamtoa katika Uislamu.
Tano: Shirki ya kimatendo: Ni kila tendo lililohukumiwa na Shari´ah ya kwamba ni shirki. Shirki hii kuna kubwa na ndogo.

Sita: Shirki ya kimatamshi: Ni kila tamshi lililohukumiwa na Shari´ah ya kwamba ni shirki. Kwa mfano kuapa kwa asiyekuwa Allaah, kama wasemavyo baadhi ya watu: ´Sikuwa mimi isipokuwa kwa ajili ya Allaah na kwa ajili yako`, ´namtegemea Allaah na wewe`, ´lau bila ya Allaah na fulani kusingelikuwa kadhaa`, na matamshi mengineyo ya shirki. Shirki hii kuna kubwa na ndogo.

Saba: Shirki ya kutunga Shari´ah: Ni mtu kuipuuza Qur-aan na Sunnah au akapuuza baadhi ya hukumu zake. Badala yake akachukua maoni na kanuni za watu. Allaah (Ta´ala) amesema:

أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ
“Je, wanao washirika waliowaamuru dini yale ambayo Allaah Hakuyatolea kwayo idhini?” (42:21)

Nane: Shirki ya mapenzi: Ni kule mtu kumpenda asiyekuwa Allaah kama jinsi anavyompenda Allaah au zaidi. Anasema Allaah (Ta´ala):

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ
“Na miongoni mwa watu wako wenye kuchukua asiyekuwa Allaah kuwa ni wanaolingana [na Allaah] wanawapenda kama mapenzi ya kumpenda Allaah.” (02:165)

Tisa: Shirki ya khofu na kuogopa: Tutalizungumzia katika “Vigawanyo vya khofu” – Allaah akitaka.

Kumi: Shirki ya makusudio na matakwa: Ni mtu afanye ´amali na huku asimkusudii na wala asifanye kwa ajili ya Allaah. Hii ni shirki ya makusudio na matakwa.

Kumi na moja: Shirki ya utiifu: Ni kule mja kumtii mtu katika kuhalalisha haramu au kuharamisha halali. Amesema (Ta´ala):

اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ
“Wamewafanya marabi na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Allaah.” (09:31)

Mwandishi: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
Chanzo: al-Qawl al-Mufiyd fiy Adillat-it-Tawhiyd
Toleo la: 15.08.2015
Tarjama: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , al-Qawl al-Mufiyd fiy Adillat-it-Tawhiyd - al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: http://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 15th, August 2015