Fataawa Mpya

Allaah (Ta´ala) amesema:

عَالِمُ الْغَيْبِ فَلَا يُظْهِرُ عَلَىٰ غَيْبِهِ أَحَدًا إِلَّا مَنِ ارْتَضَىٰ مِن رَّسُول
"Mjuzi wa ghayb na wala Hamdhihirishii yeyote ghayb Yake. Isipokuwa yule Aliyemridhia miongoni mwa Mitume." (72:26-27)

Je, walii katika Ummah wa Mtume ni mwenye kuwafuata kwa kujua mambo yaliyofichikana?

Nimesikia baadhi ya wanachuoni wetu wakisema kuwa katika Hadiyth kuna khabari yenye kusema “Qiyaamah kitakuwa baada ya karne kumi na nne na kitu”. Je, maelezo haya ni sahihi? Kwa vile kumeshapita karne kumi na nne na hakukupitika kitu.

Ni ipi hukumu ya Shari´ah kwa mtazamo wenu juu ya matamshi yafuatayo:

“Allaah anajua”, “Allaah asijaalie”, “Allaah asikadirie”, “Allaah ametaka iwe” na “Allaah na Mtume Wake ndio wanajua zaidi”?

Nimesikia baadhi ya maneno ambayo yanakaririwa na baadhi ya watu. Nilikuwa nataka kujua ni upi msimamo wa Uislamu kwa maneno haya. Kwa mfano anapokufa mtu kuna wanaosema “Marehemu fulani” - فلان المرحوم - na ikiwa ni mtu mwenye cheo kikubwa wanasema “Fulani aliyesamehewa”. Je, watu hawa wamechungulia kwenye Ubao uliohifadhiwa na kujua kuwa fulani huyo amesamehewa na fulani mwingine amerehemewa? Imekuwa watu wanachukulia usahali kuhusiana na mambo haya. Amesema (Ta´ala) katika Qur-aan:

وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ
"Pindi Alipochukua Allaah fungamano la wale waliopewa Kitabu: Bila shaka mtakibainisha kwa watu na wala hamtokificha.” (03:187)

Naomba mnipe fatwa.

Sentesi: mauti ni mamoja na sababu zinatofautiana?

Makala 5 Mpya